إعدادات العرض
Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti
Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- Ya kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti".
[Sahihi]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Русский Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Românăالشرح
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa miongoni mwa dalili za kukaribia kwa Kiyama na kumalizika kwa Dunia, ni watu kujifaharisha kwa kuipamba Misikiti yao, au kujifaharisha kwa dunia yao ndani ya misikiti ambayo haikujengwa ila kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu.فوائد الحديث
Uharamu wa kujifaharisha kwa Misikiti, na kwamba ni jambo lisilokubalika; kwa sababu kitendo hicho hakikufanyika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Katazo la kuipamba Misikiti kwa rangi na vito na nakshi, na maandishi; kwa sababu ndani yake kuna kuwashughulisha wenye kuswali wanapoyatazama.
Amesema Assanadi: Hadithi ni miongoni mwa zile ambazo uhalisia unashuhudia yaliyosemwa, ni miongoni mwa miujiza ya kushangaza ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
التصنيفات
Hukumu za Misikiti.