Hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, ikiwa mtu atasalimika nalo basi yajayo baada yake ni mepesi kuliko hili, na asiposalimika nalo basi yajayo baada yake ni magumu kuliko hili

Hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, ikiwa mtu atasalimika nalo basi yajayo baada yake ni mepesi kuliko hili, na asiposalimika nalo basi yajayo baada yake ni magumu kuliko hili

Kutoka kwa Haani, mwachwa huru wa Othmani radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Othmani anaposimama juu ya kaburi analia mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Ukikumbuka pepo na Moto wala haulii, na unalia kwa sababu ya hili (kaburi)?! Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, ikiwa mtu atasalimika nalo basi yajayo baada yake ni mepesi kuliko hili, na asiposalimika nalo basi yajayo baada yake ni magumu kuliko hili".

[Ni nzuri]

الشرح

Alikuwa kiongozi wa waumini Othmani bin Affani radhi za Allah ziwe juu yake anaposimama juu ya kaburi analia sana, mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Unakumbuka pepo na moto na wala haulii kwa shauku ya pepo wala hofu ya moto! na unalia kwa sababu ya kaburi? Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza kuwa hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, mtu akisalimika na akaepukana na mabaya yaliyomo basi vituo vinavyofuata baada yake ni vyepesi mno, na asiposalimika kutokana na adhabu zake; basi adhabu zinazofuata baada yake ni kali kuliko hizo.

فوائد الحديث

Kumebainishwa hofu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyokuwa nayo Othmani radhi za Allah ziwe juu yake, pamoja nakuwa yeye ni miongoni mwa waliobashiriwa pepo.

Sheria ya kulia wakati wa kukumbuka misukosuko ya kaburi na Kiyama.

Kumethibitishwa neema za kaburi na adhabu zake.

Tishio la adhabu za kaburi.

التصنيفات

Watu wa makaburini.