Muosheni mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, mkiona kuna haja ya kuzidisha, kwa maji na mkunazi, na mwisho muweka kafuri -au chochote katika kafuri-, mkimaliza nipeni idhini

Muosheni mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, mkiona kuna haja ya kuzidisha, kwa maji na mkunazi, na mwisho muweka kafuri -au chochote katika kafuri-, mkimaliza nipeni idhini

Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alifariki mmoja kati ya mabinti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akatoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Muosheni mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, mkiona kuna haja ya kuzidisha, kwa maji na mkunazi, na mwisho muweka kafuri -au chochote katika kafuri-, mkimaliza nipeni idhini" Anasema: tulipomaliza tulimpa idhini, akatupatia kikoi chake, akasema: "Mfunikeni kwa kikoi hiki", anasema: Na tukafanya (nywele za) kichwa chake kuwa mafungu matatu.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alifariki Zainab binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akaingia rehema na amani ziwe juu yake kwa wanawake waliotakiwa kumuosha, akasema: Muosheni kwa maji na Mkunazi kwa witiri mara tatu, au mara tano au zaidi ya hapo, ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo, na muweke katika muosho wa mwisho chochote katika kafuri, na mkimaliza nijulisheni. Walipomaliza kumuosha wakampa idhini, akawapa waoshaji kikoi chake, na akasema: Mzungushieni ndani yake na muifanye kuwa ndio nguo inayofuata mwili wake, kisha kikafanywa kichwa chake kuwa na mafungu matatu ya nywele.

فوائد الحديث

Uwajibu wa kumuosha maiti wa kiislamu, na kuwa hilo ni faradhi kifaya (wakipatikana wanaotosheleza madhambi yanawaondokea wengine).

Mwanamke haoshwi ila na wanawake wenzake, na mwanaume haoshwi ila wanaume, isipokuwa wale walioruhusiwa kama mwanamke pamoja na mume wake, na mjakazi na bosi wake, hao wote kila mmoja anaruhusiwa kumuosha mwenzake.

Josho linakuwa kwa miosho mitatu, isipotosha, basi mitano, na isipotosha, itazidishwa zaidi ya hapo, kulingana na masilahi na haja ya kufanya hivyo, na baada ya hapo ikiwa najisi itatoka katika mwili wake, itazibwa sehemu unapotoka udhia huo.

Atakamilisha muoshaji uoshaji wake kwa witiri, tatu, au tano, au saba.

Amesema Assanadi: Hakuna kikomo katika kumuosha maiti bali kinachotakiwa ni kumsafisha, lakini ni lazima kuzingatia witiri.

Maji yawe pamoja na Mkunazi; kwa sababu hutakatisha, na kuufanya mwili wa maiti kuwa mkavu.

Maiti hutiwa manukato kwa josho lake la mwisho, ili maji yasimalizike, na marashi yawe ya kafuri, kwa sababu pamoja na harufu nzuri, huukaza mwili, na kuufanya usiharibike haraka.

Kuanza kwa kuosha viungo vitukufu, navyo ni vile vya kulia, na viungo vya udhu.

Kupendeza kuchana nywele za maiti na kuzifunga mafundo matatu, na kuziweka nyuma ya maiti.

Inafaa kusaidizana katika kumuosha maiti lakini asihudhurie ila yule anayehitajika.

Kutaka baraka kupitia athari za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama mavazi yake, na hili ni jambo maalumu kwake, halivuki kwenda kwa mtu mwingine katika wanachuoni na watu wema; kwa sababu mambo hayo yanahitaji msingi wa sheria, na Maswahaba hawakuwahi kulifanya hilo na yeyote katu; na ni kwa sababu kufanywa hilo na mtu mwingine ni sababu ya kuingia katika ushirikina na fitina kwa atakayetakwa baraka.

Inafaa kumpa kazi mtu mwaminifu kwa kile alichoaminiwa kwacho, ikiwa anastahiki kupewa kazi.

التصنيفات

Kuosha Maiti.