Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea

Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwizi unakatwa mkono wake kwa kuiba robo Dinari ya dhahabu, na zaidi ya hapo, na kiwango chake kinalingana na kiasi cha Gramu 1.06 ya dhahabu.

فوائد الحديث

Wizi ni katika madhambi makubwa.

Ameweka mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu wa adhabu ya mwizi, nayo ni kukata mkono wake, kama ilivyo katika kauli yake Mtukufu: "Na mwizi mwanaume na mwizi mwanamke basi ikateni mikono yao" [Maaida: 38], na mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake yamebainisha sharti za kukata huku.

Makusudio ya mkono katika hadithi ni kukikata kiganja katika maungio yake kati yake na muundi wa mkono.

Na miongoni mwa hekima katika kukata mkono wa mwizi, ni kulinda mali za watu, na kumkomesha mtu mwingine katika watu wanaofanya uadui katika mali za watu.

Dinari ni uzito wa dhahabu, na inalingana kwa sasa na (Gramu 4.25) kwa kipimo cha 24; hivyo robo Dinari inalingana na gramu moja na kitu.

التصنيفات

Adhabu ya uwizi.