Nitampa bendera kesho mtu ambaye anampenda Allah na Mtume wake,na anapendwa na Allah na Mtume wake,kupitia yeye Allah ataleta ushindi.

Nitampa bendera kesho mtu ambaye anampenda Allah na Mtume wake,na anapendwa na Allah na Mtume wake,kupitia yeye Allah ataleta ushindi.

Kutoka kwa Sahli bin Saidi As saaidiy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Nitampa bendera kesho mtu ambaye anampenda Allah na Mtume wake, na anapendwa na Allah na Mtume wake, kupitia yeye Allah ataleta ushindi, wakalala watu wakijadiliana hilo usiku kucha, ni yupi kati yao atakayepewa, walipoamka asubuhi, wakaenda mapema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- kila mmoja kati yao akitaraji kupewa yeye: Akasema: Yuko wapi Ally bin Abii Twalib? wakasema: Anasumbuliwa na macho, wakaagiza akaletwa, akamtemea mate machoni mwake, na akamuombea, akapona kana kwamba hakua na ugonjwa, akampa bendera, akasema: nenda taratibu mpaka ushuke katika kiwanja chao, kisha waite katika uislamu na uwaeleze yaliyowajibu kwao katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, Basi Wallahi -namuapa Mwenyezi Mungu- akikuongozea Mwenyezi Mungu mtu mmoja ni bora kwako kuliko ngamia mwekundu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Kwamba Mtume -rehma na amani ziwe juu yake- aliwabashiria Maswahaba ushindi dhidi ya mayahudi tangu jana yake,kupitia mtu mwenye fadhila kubwa , na mapenzi makubwa kwa Allah na Mtume wake,wakalitamani hilo maswahaba,kila mmoja anatamani awe ni yeye, kutokana na pupa walizokuwa nazo katika mambo ya kheri, walipokwenda katika siku ya ahadi, Mtume akamtaka Ally , na ikasadifu kuwa hakuhudhuria kwa sababu anaumwa macho, kisha akahudhuria na Mtume akamtemea mchoni upepo mwepesi akimsomea dua na maumivu yakaondoka palepale, Mtume akampa jukumu la kuongoza jeshi, na akamuamuru aende asonge polepole mpaka akikaribia ngome ya maadui, awalinganie kuingia katika Uislamu,wakikubali awaelekeze yanayompasa Muislamu miongoni mwa faradhi, kisha Mtume akambainishia Ally fadhila za Da`awa, na kwamba mlinganiaji akifanikiwa kumuongoza mtu mmoja, basi hilo ni bora kwake kulikoni mali zenye thamani kubwa hapa duniani, vipi akibahatika kuwaongoa watu wengi!

التصنيفات

Tiba na kutumia dawa na Ruq'ya ya kisheria., Ubora wa Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao., Vita alivyoshriki na Ambavyo hajashiriki Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: