إعدادات العرض
Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni,
Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni,
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, na likiwa si la mtu mwema basi husema: Ubaya ulioje, mnalipeleka wapi? Huisikia sauti yake kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angelisikia basi angezimia".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî தமிழ் অসমীয়া Nederlands አማርኛ ไทยالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba Jeneza likiwekwa kitandani, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, kwa yale linayoyaona mbele yake katika neema, na likiwa si la mtu mwema, hupiga yowe kwa sauti mbaya ya kukera, na kusema: Nasikitika kwa maangamivu yake, mnalipeleka wapi?! kwa yale linayoyaona mbele yake miongoni mwa adhabu, inasikika sauti yake kwa kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angeliisikia basi angezimia kutokana na ukubwa wa kile alichosikia.فوائد الحديث
Maiti mwema huanza kuona habari njema kabla ya kuzikwa kwake, na kafiri hufadhaika, na kuona mambo kinyume na hivyo.
Baadhi ya suti husikiwa na viumbe vingine tofauti na mwanadamu, na wala mwanadamu hawezi kuzisikia.
Sunna ni kulibeba Jeneza juu ya mabeba ya wanaume na si wanawake; kwa katazo la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwakataza wanawake kusindikiza Jeneza.
التصنيفات
Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa)