إعدادات العرض
Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki
Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki
Kutoka kwa Shuraihi bin Hanii amesema: Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी සිංහල Hausa Kurdî Português Nederlands Tiếng Việt অসমীয়া ગુજરાતી አማርኛ پښتو ไทยالشرح
Ilikuwa katika muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuanza na mswaki anapoingia nyumbani kwake wakati wowote, usiku au mchana.فوائد الحديث
Sheria ya kupiga mswaki ni ya ujumla kwa nyakati zote, na inatiwa mkazo: katika nyakati ambazo sheria imehimiza, miongoni mwake ni: Wakati wa kuingia nyumbani, na wakati wa swala, na wakati wa udhu, na baada ya kuamka kutoka usingizini, na wakati wa kubadilika kwa harufu ya kinywa.
Kumebainishwa pupa ya wanafunzi wa Maswahaba ya kuuliza kuhusu hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na sunna zake; ili wamuige.
Kuchukua elimu kutoka kwa wenye elimu na kwa wale wenye kujua zaidi, kiasi ambacho aliulizwa Aisha kuhusu hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kuingia kwake nyumbani.
Uzuri wa maisha ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na familia yake, kiasi kwamba alikuwa akisafisha kinywa chake wakati wa kuingia.
التصنيفات
Sunna za Kimaumbile.