Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi (lingeyabadili rangi) kwa kuchanganyika nayo

Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi (lingeyabadili rangi) kwa kuchanganyika nayo

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Inakutosha kwa Safia kadhaa wa kadhaa, (Anasema mmoja wa wapokezi wa hadithi hii: Alikuwa akikusudia ufupi) Akasema: "Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi (lingeyabadili rangi) kwa kuchanganyika nayo" Akasema Aisha: Na nikamsimulia kuhusu mtu fulani, akasema: "Sipendi kuona kuwa kuna mtu nimemsimulia na kwamba mimi nina kadhaa wa kadhaa".

[Sahihi]

الشرح

Mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake alisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Inakutosha kwa Safia (Alikuwa akikusudia mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake) Kuwa miongoni mwa aibu zake za kimaumbile ya kimwili ni mfupi, Mtume akasema: Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi lingeyazidia na kuyabadili na kuyaharibu, Aisha akasema: Na nilichokifanya ni sawa na kitendo cha mtu kumsema mtu ili kumshusha hadhi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Sipendezwi kuzungumza aibu zake, au kusimulia kuhusu yeye au kufanya mfano wa vitendo vyake, au kusema mfano wa kauli zake, kwa sura ya kumdharau hata kama nitapewa kiasi kingi katika mali za dunia kwa hilo.

فوائد الحديث

Tahadhari na kitisho dhidi ya kusengenya.

Kuigiza mionekano na kuwasimuliza watu kwa njia ya kudharau na kushusha hadhi ni katika usengenyaji ulioharamishwa.

Kueleza wasifu wa aibu za kimwili ni sehemu katika usengenyaji.

Amesema Kadhi: Kuchanganya na kubadili na kuunganisha kitu na kingine, na maana yake ni kuwa utesi huu lau ungelikuwa ni katika vitu vinavyochanganyikana na Bahari basi ungeibadili kutoka katika hali yake, pamoja na wingi, ni vipi ukiwa katika amali ndogo kisha ukachanganyika nazo!.

Hapa kumeelezwa sehemu miongoni mwa mambo yanayotokea kati ya wana ndoa wawili miongoni mwa wivu.

Kutokubaliana kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na uovu.

Kuifanya dunia kuwa ndogo pamoja na vyote vilivyomo pale inapolinganishwa na radhi za Allah Mtukufu na kutokasirika kwake.

Uislamu ni dini ya tabia njema, na umeamrisha kuhifadhi heshima zisije kuvunjwa kwa kauli au kitendo; kwa sababu hilo ni miongoni mwa mambo yanayopandikiza chuki na uadui kati ya waislamu.

التصنيفات

Tabia mbovu.