Asife mmoja wenu isipokuwa naye awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Mtukufu

Asife mmoja wenu isipokuwa naye awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Mtukufu

Kutoka kwa Jabir bin Abdillahi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kabla ya kifo chake kwa siku tatu akisema: "Asife mmoja wenu isipokuwa naye awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Mtukufu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Jambo la wajibu kwa Muislamu aishi baina yakuwa na hofu na matumaini, hofu ya ghadhabu za Mwenyezi Mungu na hasira zake, na matumaini ya kupata msamaha wake na rehema zake, lakini wakati wa kuvuta hisia upande wa matumaini uzidi, na azidishe kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, na ataraji na ategemee rehema yake na msamaha wake, mpaka liwe hilo ni kizuizi cha yeye kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu kwa wakati huo.

التصنيفات

Matendo ya moyoni.