إعدادات العرض
Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa kuni juu ya mgongo wake, akauuza, na Mwenyezi Mungu akausitiri uso wake, basi hilo ni bora zaidi kwake kuliko kuwaomba watu wampe au wamnyime
Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa kuni juu ya mgongo wake, akauuza, na Mwenyezi Mungu akausitiri uso wake, basi hilo ni bora zaidi kwake kuliko kuwaomba watu wampe au wamnyime
Kutoka kwa Zubair bin Awwam -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa kuni juu ya mgongo wake, akauuza, na Mwenyezi Mungu akausitiri uso wake, basi hilo ni bora zaidi kwake kuliko kuwaomba watu wampe au wamnyime"
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Tiếng Việt Português Magyar ქართული සිංහල Română অসমীয়াالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu anapofanya kazi yoyote hata kama ni kuchukua kamba, akaitumia kukusanyia kuni juu ya mgongo wake, akaziuza na akapata chakula kwa hilo, au akatoa sadaka, na akajitosheleza na kutowaomba watu na akaulinda uso wake na udhalili wa kuombaomba; hilo ni bora zaidi kwake kuliko kuwaomba watu, ima wampe au wamnyime, kuwaomba watu ni udhalili, na muumini anaheshima na wala si dhalili.فوائد الحديث
Himizo la kujizuia kuomba na kujitakasa na hilo.
Himizo la kufanya kazi kwa ajili ya kupata riziki, hata kama mtu mzima atafanya kazi ndogo na ya udhalili katika macho ya watu.
Vita ya Uislamu dhidi ya kuombaomba na kubweteka; na ndio maana umewajibisha kwenda mbio na kufanya kazi, hata kama itakuwa ngumu; kama kuchanja kuni kwa mfano.
Si halali kuomba, mtu akiwa na uwezo wa kufanya kazi na kujitafutia riziki.
Kumuomba kiongozi kukiwa na haja inafaa, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala wale waliokujia ili uwachukue ukasema: Sina kipando cha kukuchukueni. Tena wakarudi na macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa cha kutoa." [Tauba: 92]
Atakayedharurika kuomba na akawa dhaifu hawezi kujitafutia riziki na kuchanja kuni, basi inafaa kwake kuomba, lakini asing'ang'anie na kulazimisha, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hawang'ang'anii watu kwa kuwaomba" [Al-Baqara: 273].
Amesema Nawawi: Hapa: Kuna himizo la kutoa sadaka, na mtu kula kwa chumo la mkono wake, na kutafuta riziki ya halali.
التصنيفات
Biashara.