Nilimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni dhambi ipi kubwa zaidi mbele ya Allah? Akasema: "Ni wewe kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na hali yeye ndiye aliyekuumba

Nilimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni dhambi ipi kubwa zaidi mbele ya Allah? Akasema: "Ni wewe kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na hali yeye ndiye aliyekuumba

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni dhambi ipi kubwa zaidi mbele ya Allah? Akasema: "Ni wewe kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na hali yeye ndiye aliyekuumba" Nikasema: Hakika hilo ni jambo kubwa, nikasema: Kisha ipi? Akasema: "Na kumuua mwanao; ukiogopea atakula pamoja nawe" Nikasema: Kisha ipi? Akasema: "Ni wewe kumzini mke wa jirani yako".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu dhambi kubwa akasema: Kubwa zaidi ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, nako ni kumuwekea Mwenyezi Mungu mfano katika uungu wake au uumbaji wake au majina yake na sifa zake, na dhambi hili halisamehe Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa toba, na akifa mfanyaji wake huyo atakaa milele motoni. Kisha ni mtu kumuua mwanaye kwa kuchelea kula naye, na kuua nafsi ni haramu, lakini dhambi linakuwa kubwa pale anapokuwa muuliwaji ni ndugu wa damu wa muuaji, na dhambi lake linakuwa kubwa pia pale linapokuwa lengo la muuaji ni kuchelea kushirikiana pamoja na muuliwaji katika riziki ya Mwenyezi Mungu. Kisha ni mtu kumzini mke wa jirani yake kwa kujaribu kumhadaa mke wa jirani yake mpaka akafikia kuzini naye, naye akamkubalia, Na zinaa ni haramu lakini dhambi lake linakuwa kubwa anapokuwa mziniwa ni mke wa jirani ambaye sheria imeusia kumtendea wema na kuishi naye vizuri.

فوائد الحديث

Kutofautiana ukubwa kwa madhambi, kama ambavyo matendo mema yanazidiana katika ubora.

Dhambi kubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha kumuua mtoto kwa kuchelea kula naye, kisha kumzini mke wa jirani yako.

Riziki iko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, na amechukua jukumu -Aliyetakasika- la kuwaruzuku viumbe.

Ukubwa wa haki ya jirani, nakuwa kumuudhi ni dhambi kubwa kuliko kumuudhi mwingine.

Muumba ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa yeye peke yake asiye na mshirika wake.

التصنيفات

Kumpwekesha Allah kwa vitendo vyake(Uumbaji)