Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono

Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono

Kutoka kwa Maliki bin Ausi bin Hadathani yakuwa yeye alisema: Niligeuka nikasema ni nani anayechenji pesa? Twalha bin Ubaidillah akasema wakati akiwa kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yao wote: Tuonyeshe Dhahabu yako, kisha tuletee, atakapokuja mfanyakazi wetu tutakupa pesa yako, akasema Omari bin Khattwab: Hapana, ni lazima utampa haki yake, au umrejeshee Dhahabu yake, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Taabii (Mwanafunzi wa Maswahaba) Malik bin Ausi anaeleza kuwa alikuwa na dinari za dhahabu, na alitaka kuzibadilisha kwa dirham za fedha, basi Twalha bin Ubaidillah (radhi za Allah ziwe juu yake) akamwambia: Tupe dinari zako nizione! Kisha akamwambia baada ya kuamua kununua: Njoo kwetu ikiwa mtumwa wetu atakuja baadaye tutakupe dirham za fedha, Omari bin Khattab Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alilaani aina hii ya muamala (biashara), na akaapa kwa Twalha kuwa atalipa fedha sasa, au amrudishie dhahabu yake aliyoichukua yeye, akasema kuwa kuuza fedha kwa dhahabu, au kinyume chake, lazima kupokea kuwe mkono kwa mkono, vinginevyo biashara hiyo itakuwa ni riba iliyoharamishwa na uuzaji batili, Dhahabu haiuzwi kwa fedha, wala fedha kwa dhahabu, isipokuwa mkono kwa mkono, na kufanyike kubadilishana, wala haiuzwi kwa ngano, na shayiri kwa shayiri, na tende kwa mfano wake, kipimo kwa kipimo, mkono kwa mkono; na haijuzu kuachana katika makubaliano kabla ya kuimiliki.

فوائد الحديث

Kuna aina tano za vitu vilivyotajwa katika Hadith hii: dhahabu, fedha, ngano, shayiri, na tende Ikiwa uuzaji utafanyika katika kundi moja, masharti mawili lazima yatimizwe kwa ajili ya uhalali wake: kubadilishana katika kikao cha mkataba, na kufanana katika aina na uzito, kama vile dhahabu kwa dhahabu, vinginevyo itakuwa ni riba ya mkopo, na ikiwa ni tofauti mnavyouziana kama vile fedha na ngano kwa mfano, basi ili kusihi biashara hii linahitajika sharti moja wakati wa mkataba, vinginevyo itakuwa ni riba ya mkopo.

Makusudio ya kikao cha makubaliano: Ni mahala pa kuuziana, sawa sawa wawe wamekaa au wanatembea, au wamepanda, na makusudio ya kuachana ni kila namna ya kuachana waliyoizoea watu.

Katazo katika Hadithi linakusanya aina zote za dhahabu zilizosafishwa na ambazo hazijasafishwa, na aina zote za fedha, zilizosafishwa na zinginezo.

Miamala ya kifedha ya zama hizi ni wajibu kufanyika kilichowajibu katika biashara ya dhahabu na fedha, yaani endapo utataka kubadili fedha ya noti au sarafu kwa fedha nyingine ya noti au sarafu, kama Riyal kwa Dirham au Shilingi kwa Dollar, hapa inajuzu kupishana thamani kwa namna watakavyoelewana pande zote mbili, lakini ni wajibu kukabidhiana katika kikao cha mauziano, vinginevyo mauziano yatakuwa batili, na muamala huu utakuwa umeingia katika Riba iliyoharamishwa.

Miamala yote ya riba haifai, na makubaliano yake ni batili hata kama wataridhiana pande zote mbili; kwa sababu Uislamu unahifadhi haki ya mtu na ya Jamii nzima kwa ujumla, hata kama yeye mwenyewe atakubali haki yake iende.

Kukataza uovu na kuuzuia kwa atakayeweza kulifanya hilo.

Kutaja ushahidi wakati wa kukemea uovu, kama ilivyotokea kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake.

التصنيفات

Riba.