إعدادات العرض
Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake
Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Kiongozi muadilifu, na kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu, na mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika misikiti, na watu wawili walipoendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakakutana kwa ajili yake na wakaachana kwa ajili yake, na mwanaume aliyeitwa na mwanamke mwenye wadhifa na uzuri, akasema: Hakika mimi ninamhofu Allah, na mtu aliyetoa sadaka akaificha mpaka usijue kushoto kwake unachotoa kulia kwake, na mtu aliyemkumbuka Mwenyezi Mungu akiwa faragha, yakabubujika machozi macho yake".
الشرح
Alitoa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya aina saba za waumini atakaowapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kivuli cha Arshi yake siku ambayo hakutokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Wa kwanza: Imamu muadilifu katika nafsi yake na si muovu, na ni muadilifu kwa raia wake na si dhalimu; naye ni yule mwenye mamlaka ya juu, na anaungana naye kila kiongozi atakayeongoza chochote katika mambo ya waislamu akafanya uadilifu ndani yake. Wa pili: Ni kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu, na akaumaliza ujana wake na uchangamfu wake, mpaka akafishwa katika hali hiyo. Wa tatu: Ni mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika msikiti, pindi akitoka mpaka hatulizani mpaka arudi ndani yake kwa sababu ya mapenzi makubwa na wingi wa kushikamana na msikiti na kuendelea kubaki ndani yake kwa moyo, hata kukitokea dharura akiwa msikitini akatoka nje ya msikiti. Wa nne: Ni watu wawili kila mmoja alimpenda mwenzake kweli kweli kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wakadumu katika mapenzi ya dini na ikawa haikuwakatisha sababu yoyote ya kidunia zaidi kukutana kweli au la sivyo mpaka kifo kikawatenganisha. Wa tano: Na mwanaume aliyetakwa na mwanamke ili kumtumia kufanya machafu, naye ni mwanamke mwenye msingi mzuri na heshima na ukoo mtukufu na cheo na mali na uzuri, akakataa na akasema kumwambia: Hakika mimi ninamuhofu Allah. Wa sita: Ni mtu aliyetoa sadaka ndogo au nyingi, na hakutaka kuonekana ndani yake, bali aliificha mpaka haukujua mkono wa koshoto kwake kilichotolewa na mkono kulia kwake. Wa saba: Ni mtu aliyemtaja Mwenyezi Mungu kwa moyo wake kwa kumkumbuka, au kwa ulimi wake kwa kufanya dhikri, akiwa faragha mbali na watu, yakabubujika machozi kutoka machoni mwake kwa hofu na kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu.فوائد الحديث
Fadhila za makundi saba yaliyotajwa na himizo la kuyaiga.
Amesema bin Hajari katika kauli yake "Katika kivuli chake": Imesemwa kuwa makusudio yake: Ni kivuli cha Arshi yake, na linaonyeshwa hilo na hadithi ya Salmaan iliyoko kwa Saidi bin Mansuri kwa Isnadi hasan "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu chini ya kivuli cha Arshi yake".
Amesema bin Hajari: Na tafsiri nzuri iliyofasiriwa neno muadilifu: Ni yule anayefuata amri za Mwenyezi Mungu kwa kukiweka kila kitu mahali pake, pasina uzembe wala kupita mpaka, na amemtanguliza katika kumtaja kwa sababu ya manufaa yake mapana.
Fadhila za kusubiri swala baada ya swala.
Amesema Nawawi: Hapa kuna himizo la kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kumebainishwa ukubwa wa fadhila zake.
Umetajwa wadhifa na uzuri pekee kwa sababu ya shauku kubwa ya watu katika hayo, na kuyapupia kwao, na ugumu wa kupatikana kwake.
Kilicho bora katika sadaka ni kuficha na kujiweka mbali na kujionyesha, pamoja nakuwa ni sheria kudhihirisha sadaka na zaka, ikiwa zitasalimika na kujionyesha, na zikakusudiwa kuwahimiza wengine katika utoaji na ili mtu mwingine amuige, na kwa ajili ya kudhihirisha nembo ya Uislamu.
Na bila shaka wamepata watu hao neema hiyo kwa sababu ya kutakasa nia zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwenda kinyume na matamanio ya nafsi.
Kauli yake: "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu": Kuwadhibiti kwa idadi hii si lengo, bali imepokelewa watu wengine wasiokuwa hawa katika hadithi nyingine miongoni mwa wale atakaowakinga Mwenyezi Mungu chini ya kivuli cha Arshi yake.
Amesema bin Hajari: Kutajwa wanaume pekee katika hadithi hii haina maana yoyote; bali wanawake wanashirikiana nao katika matendo yaliyotajwa, isipokuwa kama itakuwa makusudio ya kiongozi muadilifu ni uongozi mkuu, na kama si hivyo basi kunauwezekano wa mwanamke pia kuingia katika hili pale anapokuwa na familia akawafanyia uadilifu, na anaondolewa katika swala la kudumu msikitini; kwa sababu swala ya mwanamke nyumbani kwake ndiyo bora kuliko kuswalia msikitini, na mbali na hayo basi yaliyobakia yote wanashirikiana na yanapatikana kwao, hata mwanaume aliyeitwa na mwanamke, hili pili linaweza kutokea kwa mwanamke aliyeitwa na mfalme mzuri kwa mfano akakataa kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na kuwa anamuhitajia.