إعدادات العرض
Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa
Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa
Kutoka kwa Abuu Umama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa".
[Sahihi]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português دری অসমীয়া Tiếng Việt አማርኛ Svenska ไทย Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી नेपाली Română മലയാളം Nederlands Oromoo සිංහල తెలుగు پښتو Soomaali Kinyarwanda Malagasy ಕನ್ನಡ Српски Moore ქართულიالشرح
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema kuwa mwenye kusoma Ayatul-Kursi baada ya kumalizika kwa swala ya faradhi, hakuna kitakachomzuia kuingia Peponi isipokuwa kifo; nayo iko katika Suratul Baqarah, Mwenyezi Mungu anasema: "Mwenyezi Mungu - hapana mungu isipokuwa Yeye, Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hashikwi na kusinzia wala kulala. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Ni nani huyo awezaye kufanya uombezi mbele yake isipokuwa kwa idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui vyema chochote katika elimu yake isipokuwa kwa kile akitakacho. Kuti chake cha enzi kimeenea mbingu na dunia, na wala halemewi na kuvilinda vyote viwili. Na Yeye ndiye aliye juu zaidi, Mkuu." [Al-Baqara: 255]فوائد الحديث
Fadhila ya Aya hii tukufu; kwa kukusanya kwake majina mazuri, na sifa za hali ya juu.
Sunna ya kusoma Aya hiyo tukufu baada ya swala za faradhi.
Matendo mema ni sababu ya kuingia peponi.