إعدادات العرض
Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili
Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake-: Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili, atapochelea Alfajiri aswali rakaa moja, iwe ni witri kwa aliyo swali" na yeye alikuwa akisema: "Fanyeni swala yenu ya mwisho iwe ni witri", kwa hakika Mtume rehema na amani za Allah zimshukie kaamrisha hivyo.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو हिन्दी 中文 Tiếng Việt ئۇيغۇرچە Kurdî Português دری Македонски Magyar ქართული ไทย অসমীয়া Hausa Nederlands ਪੰਜਾਬੀالشرح
Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa anahutubia juu ya Mimbari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nifundishe ni namna gani nitaswali usiku?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utaswali na kutoa salamu katika kila rakaa mbili, ukihofia kuchomoza kwa Afajiri basi swali rakaa moja itakufanyia kuwa witiri rakaa zingine ulizoswali, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiusia kuifanya swala ya mwisho ya usiku kuwa ni witiri.فوائد الحديث
Asili katika swala za usiku ni mtu atoe salamu katika kila rakaa mbili, nje na witiri.
Nikuwa swala za usiku hazina idadi maalumu; kwa kuwa tamko liliachwa wazi.
Amesema Nawawi: "Swala za usiku na mchana ni rakaa mbili mbili", hadithi hii inachukuliwa kama kubainisha kilicho bora zaidi, nayo ni atoe salamu katika kila rakaa mbili, na sawa sawa ziwe ni sunna za usiku na mchana, na ni sunna atoe salamu kwa kila rakaa mbili.
Amesema Nawawi: Hapa kuna ushahidi kuwa sunna ni kuifanya witiri kuwa swala ya mwisho wa usiku, na kwamba wakati wake unamalizika kwa kuchomoza Alfajiri, na ndio kauli mashuhuri katika madhehebu yetu, na ndivyo lilivyosema jopo la wanachuoni.
التصنيفات
Kisimamo cha Usiku.