La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu

La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa jambo la kwanza litakalohukumiwa baina ya watu katika dhulma zao wao kwa wao siku ya Kiyama: Itakuwa katika damu, kama kuua na kujeruhi.

فوائد الحديث

Ukubwa wa swala la damu, kwani siku zote jambo muhimu zaidi ndio hutangulizwa.

Dhambi huwa kubwa kulingana na madhara yanayojitokeza, na kuua nafsi isiyo na hatia ni katika madhara makubwa na hakuna kubwa zaidi yake isipokuwa ukafiri na kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التصنيفات

Maisha ya Akhera., Kisasi.