إعدادات العرض
Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu
Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî Tiếng Việt Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Românăالشرح
Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwenda mbio kuliandaa jeneza na kuliswalia na kuzika; jeneza likiwa jema basi mnaliwahisha kwenda katika kheri miongoni mwa neema za kaburi, na likiwa kinyuume na hivyo, basi hiyo ni shari mnaiweka katika shingo zenu.فوائد الحديث
Amesema bin Hajari: Inapendeza na ni sunna kwenda haraka, lakini kwa kiwango ambacho si cha nguvu, kiasi ambacho yanaweza kuhofiwa madhara kwa maiti, au uzito kwa mbebaji au msindikizaji.
Hapa kuna mpaka katika uharaka, ni pale ikiwa kifo kitakuwa cha ghafla, kwani inahofiwa inaweza kuwa ni kuzimia tu, hapa ni inatakiwa asizikwe ila baada ya kuthibitsha kifo chake, au inaweza kuwa kuchelewesha kidogo kwa ni kwa sababu ya masilahi, kama kuongezeka wa kumswalia, au kuhudhuria ndugu zake wa karibu, endapo hatohofiwa kuharibika.
Himizo la kulipeleka haraka jeneza ni kwa ajili ya masilahi ya maiti akiwa ni mtu mwema, au kwa ajili ya masilahi ya wasindikizaji akiwa ni mtu muovu.
Amesema Nawawi: Na inachukuliwa faida hapa kuwa mtu aache kusuhubiana na watu waovu wasiokuwa wema.
التصنيفات
Kumbeba maiti na kumzika.