Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.”

Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.”

Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.” Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunakuamini wewe na ulicholeta, je unatuhofia? Akasema: "Ndio, nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, anazigeuza kwa namna atakavyo"

[Sahihi]

الشرح

Dua nyingi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilikuwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu uthabiti katika dini na utiifu, na kujiepusha na kupinda na upotofu. Anas bin Malik radhi za Allah ziwe juu yake alistaajabu kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiiomba dua hii mara kwa mara, basi Mtume rehema na amani zimshukie akamwambia kuwa nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, huzigeuza apendavyo, hivyo, moyo ni kituo cha imani na ukafiri, na moyo umeitwa Qalbu kwa sababu ya kugeukageuka kwake mara kwa mara, moyo hugeuka sana kuliko chungu kinapokusanyika kile kinachotokota ndani yake. Amtakaye Mwenyezi Mungu huudumisha moyo wake katika uongofu na uthabiti katika Dini, na anayemtaka Mwenyezi Mungu huugeuza moyo wake kutoka katika uongofu na kuupeleka katika upotofu.

فوائد الحديث

Kujisalimisha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na kunyenyekea kwake, na kuuelekeza umma kuliomba hilo.

Umuhimu wa kuwa na msimamo na uthabiti katika dini, na kuwa kinachozingatiwa ni hatima ya mtu ya maisha yake.

Mja hawezi kujitosheleza mwenyewe hata kwa kupepesa jicho bila ya kutiwa uthabiti na Mwenyezi Mungu katika Uislamu.

Himizo la kuomba dua hii kwa wingi, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Kudumu katika Uislamu ni neema kubwa ambayo mja anatakiwa kuifanyia juhudi na kumshukuru Mola wake Mlezi.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume., Matendo ya moyoni.