Atakayewalea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya kiyama mimi na yeye ni kama vidole hivi viwili

Atakayewalea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya kiyama mimi na yeye ni kama vidole hivi viwili

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Atakayewalea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya kiyama mimi na yeye ni kama vidole hivi viwili" Na akashikanisha vidole vyake.

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Katika hadithi hii kuna ubora wa mtu kuwalea watoto wa kike, na hii ni kwasababu bint hajiwezi na ni dhaifu, na mara nyingi nikuwa ndugu zake huwa hawamjali, wala hawamtilii maanani, na kwasababu hii akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: ""Atakayewalea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya kiyama mimi na yeye ni kama vidole hivi viwili" Na akashikanisha vidole vyake: kidole cha shahada na cha katikati, na maana yake nikuwa yeye atakuwa rafiki yake na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- peponi atakapo walea mabinti wawili au dada wawili au wengineo, yaani yeye atakuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- peponi, na akakutanisha kati ya vidole vyake -Ziwe juu yake Rehema na Amani- na kuwalea mara nyingi huwa ni kusimamia mahitaji ya mwili, kuanzia kuvaa kula kunywa kulala na mfano wa hayo, na vile vile huwa kwa kuwasomesha na kuwapa maadili na maelekezo na kuwaamrisha mambo ya kheri na kuwakataza mambo ya shari na mengineyo, anajikuta mwenye kusimamia malezi ya mabinti kapata maslahi ya haraka ya dunia na ya baadaye ya akhera.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema.