“Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa

“Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: “Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa, ndani yake aliumbwa Adam, na ndani yake aliingizwa Peponi, na ndani ya siku hii akatolewa humo, na hakitosimama Kiyama ila siku ya Ijumaa".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake anatueleza kuwa siku bora kabisa iliyochomozewa na jua ni Ijumaa, Miongoni mwa sifa zake: Mwenyezi Mungu alimuumba Adam, amani imshukie, na ndani yake akamuingiza Peponi, na ndani yake akamtoa na akamteremsha duniani, na Kiyama hakitosimama ila siku ya Ijumaa.

فوائد الحديث

Ubora wa siku ya Ijumaa kwa siku zingine za wiki.

Himizo la kukithirisha amali njema siku ya Ijumaa, na kujiweka tayari kwa ajili ya kupata rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuzuia adhabu zake.

Sifa hizi za siku ya Ijumaa zilizotajwa katika Hadithi zilisemekana kuwa ni kutotaja fadhila ya Ijumaa; Kwa sababu kutolewa Adam peponi na kusimama Kiyama hakuzingatiwi kuwa ni neema, na imesemekana: Bali yote hayo ni neema, na kutoka kwa Adam peponi ndio sababu ya kuwepo kizazi wakiwemo Mitume na Manabii na watu wema, na kusimama kwa Kiyama ndio sababu ya kuharakishwa malipo ya watu wema na kupata yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu miongoni mwa takrima.

Sifa nyingine za ijumaa zilitajwa zaidi ya hizo zilizotajwa katika riwaya hii, ni pamoja na: ndani yake Adam alitubia, na ndani yake alifishwa, na ndani yake kuna saa ambayo hakuna mja Muumini atakaye afikiana nayo akiwa anaswali na kumuomba Mwenyezi Mungu jambo lolote isipokuwa humpa hilo analoomba.

Siku bora ya mwaka ni Siku ya Arafa, na inasemekana: Ni siku ya kuchinja, siku bora ya wiki ni Ijumaa, na usiku bora ni Laylatul-Qadri (Usiku wenye cheo).

التصنيفات

Manabii na Mitume waliotangulia - juu yao amani.