إعدادات العرض
Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha
Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî தமிழ் Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી Magyar ქართული Românăالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kuna baadhi ya watu wana nywele zilizoshikana tena zilizojaa vumbi, na hawazipaki mafuta wala hajali kuziosha, na wala hawana heshima yoyote mbele za watu, basi watu humsukuma mtu kama huyu katika milango yao, na kumfukuza kwa kumdharau; isipokuwa mtu huyu lau angeapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa litokee jambo basi Mwenyezi Mungu angelitenda jambo hilo kwa sababu ya kumkirimu na kumtukuza kwa kujibu ombi lake, na kumlinda asijekupotoka katika kiapo chake, na hii ni kwa sababu ya ubora wake na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu.فوائد الحديث
Mwenyezi Mungu hatazami sura ya mja, lakini anatazama ndani ya nyoyo na matendo.
Ni jukumu la kila mtu kuyapa kipaumbele matendo yake na usafi wa moyo wake zaidi kuliko kuutilia maanani mwili wake na mavazi yake.
Kujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu na kujidhalilisha kwake ni sababu ya kujibiwa dua, na ndiyo maana; Mwenyezi Mungu hukiepusha kuanguka patupu kiapo cha wachamungu na wenye maisha duni.
Kumebainishwa malezi ya kiutume kwa watu; ili wasidharauliane wao kwa wao.
التصنيفات
Ubora na fadhila za matendo mema.