Atakayependa Mwenyezi Mungu amuokoe na Matatizo ya siku ya Kiyama, basi amtatulie shida mwenye hali ngumu au ampunguzie

Atakayependa Mwenyezi Mungu amuokoe na Matatizo ya siku ya Kiyama, basi amtatulie shida mwenye hali ngumu au ampunguzie

Kutoka kwa Abuu Qatada radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye siku moja alimtafuta mdai wake, akajificha, kisha akampata, akasema: Hakika mimi nina hali ngumu, akasema: Je, unamuapa Mwenyezi Mungu juu ya hilo? Akasema: Ndio, ninamuapa Mwenyezi Mungu juu ya hilo. Akasema: Kwani mimi nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayependa Mwenyezi Mungu amuokoe na Matatizo ya siku ya Kiyama, basi amtatulie shida mwenye hali ngumu au ampunguzie".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Abuu Qatada Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akimtafuta mdaiwa wake aliyekuwa akijificha, akampata, mdaiwa akasema: Mimi nina hali ngumu, na sina mali ya kulipa deni lako. Abuu Qatada radhi za Allah ziwe juu yake akamtaka aape kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa hana mali? Akaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli katika hayo anayoyasema. Akasema Abuu Qatada radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Atakayependezwa na akafurahishwa kuwa Mwenyezi Mungu amuokoe na misukosuko ya siku ya Kiyama na matatizo yake na vitisho vyake, basi amtatulie shida mwenye hali ngumu, kwa kumpa muda mrefu na acheleweshe kumdai deni lake, au apunguze sehemu ya deni au amsamehe deni lote.

فوائد الحديث

Inapendeza kumpa muda mwenye hali ngumu mpaka atakapopata wepesi, au kumpunguzia deni lote au baadhi yake.

Atakayemtatulia muumini sehemu katika matatizo ya dunia basi naye Mwenyezi Mungu atamtatulia sehemu katika matatizo ya siku ya Kiyama, na malipo huenda sawa matendo.

Kanuni: Faradhi ni bora kuliko sunna, lakini katika baadhi ya nyakati sunna huwa bora kuliko faradhi, na kumuondolea deni mwenye hali ngumu ni sunna, na kumvumilia na kuacha kumdai ni faradhi, na hapa sunna ni bora kuliko faradhi.

Hadithi hii ni kwa yule mwenye hali ngumu ya kimaisha, huyu ndiye anayepewa udhuru, ama kumzungusha mtu anayekudai hali yakuwa una mali, imekuja kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Ucheleweshaji wa kulipa deni kwa mtu mwenye uwezo ni dhulma".

التصنيفات

Kukopesha.