Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani

Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani

Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufanya juhudi kuutafuta usiku wenye cheo kwa kuzidisha amali njema, nao hutarajiwa zaidi kupatikana katika siku za witiri za siku kumi za mwisho wa Ramadhani kila mwaka, nazo ni: Ishirini na moja, na ishirini na tatu, na ishirini na tano, na ishirini na saba, na ishirini na tisa.

فوائد الحديث

Fadhila za usiku wenye cheo (Lailatul-Qadri) na himizo la kuutafuta.

Katika hekima za Mwenyezi Mungu na rehema zake aliuficha usiku huu ili watu wafanye jitihada katika ibada, kwa ajili ya kuutafuta, ili zikithiri thawabu zao.

Usiku wenye cheo uko katika kumi la mwisho la Ramadhani, na katika siku za witiri ndio hutarajiwa zaidi.

Usiku wenye cheo ni moja kati ya siku za kumi la mwisho la Ramadhani, nao ndio usiku ambao Mwenyezi Mungu aliiteremsha Qur'ani ndani yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akaufanya usiku huu kuwa ni bora kuliko miezi elfu moja katika baraka zake, na utukufu wa heshima yake, na athari ya matendo mema ndani yake.

Umeitwa kuwa ni usiku wa Lailatul-Qadri, kwa kuiwekea sakna dali, ima ni kwa sababu ya utukufu wake, husemwa: Fulani anacheo kikubwa, inakuwa kuuambatanisha usiku ni katika sehemu ya kuambatanisha kitu katika sifa yake, yaani usiku mtukufu, yaani unacheo kikubwa kwa utukufu na thamani na nafasi mpaka mwisho wake, "Hakika sisi tumeiteremsha katika usiku wenye baraka" [Ad-Dukhan: 3]. Na ima imetokana na kukadiria: Inakuwa kuambatanishwa kwake ni kuambatanishwa kwa kuambatana na kile kinachokizunguka, yaani ni usiku ambao ndani yake kunakuwa na makadirio ya yale yatakayoendelea katika mwaka mzima, "Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima" [Ad-Dukhan: 4].

التصنيفات

Masiku kumi ya mwisho wa mwezi wa Ramadhani.