Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu

Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu

Kutoka kwa Ma'qal bin Yasari -radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati za vurugu na fitina na mauaji na kuparaganyika kwa mambo ya watu katika ibada na kushikamana nayo, na kwamba malipo yake ni kama kuhama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni kwa sababu watu hughafilika nayo, na hawatengi muda ila mtu mmoja mmoja.

فوائد الحديث

Himizo la kufanya ibada na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu nyakati za fitina; kwa ajili ya kujilinda na fitina, na kujihifadhi na ufisadi.

Kumebainishwa fadhila za kufanya ibada nyakati za fitina na nyakati za watu kughafilika.

Inapaswa kwa muislamu ajitenge mbali na mazingira ya fitina na kughafilika.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema.