إعدادات العرض
Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama
Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama
Imepokelewa kutoka kwa Abud-dardaa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Hausa Kurdî Português தமிழ் অসমীয়া ગુજરાતી Nederlands አማርኛ മലയാളം Română ไทยالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kukithirisha laana kwa mtu asiyestahiki huyu anastahiki kupata adhabu mbili. Ya kwanza: Hatokuwa shahidi siku ya Kiyama juu ya umma kwa mitume wao kufikisha ujumbe kwao, na wala haukubaliki ushahidi wake duniani; kwa sababu ya uovu wake, na wala hatoruzukiwa shahada, nako ni kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ya pili: Hatopewa nafasi ya kutoa utetezi siku ya Kiyama wakati ambapo waumini wataomba utetezi kwa ndugu zao waliostahiki moto.فوائد الحديث
Uharamu wa kutoa laana, nakuwa kukithirisha hilo ni dhambi miongoni mwa madhambi makubwa.
Adhabu iliyotajwa katika hadithi inamuhusu anayekithirisha kulaani, si wa mara moja na mfano wake, kwa sababu kwake pia kunatoka laana za halali, nazo ni zile ambazo sheria imekuja kuwalaani watu wenye sifa mbaya pasina kumuainisha mtu, kama kusema: "Mwenyezi Mungu awalaani Mayahudi na Wakristo", "Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya madhalimu" Mwenyezi Mungu amewalaani wanaopiga picha", "Mwenyezi Mungu amemlaani atakayefanya vitendo vya watu wa Luti", "Mwenyezi Mungu amemlaani atakayechinja kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu", "Mwenyezi Mungu amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake, na wanawake wenye kujifananisha na wanaume", na mfano wa hizo.
Kumethibitishwa uombezi wa waumini siku ya Kiyama.
التصنيفات
Tabia mbovu.