Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani

Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani

Kutoka kwa Abdullah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alipokuja Madina Mtume rehema na amani ziwe juu yake, watu walikusanyika mbele yake, pakasemwa: Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakasema mara tatu, nikaja pamoja na watu kutazama, na nilipouona uso wake nikajua kuwa uso wake si uso wa muongo, kwa hivyo jambo la kwanza nililomsikia akizungumza alisema kuwa: "Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".

[Sahihi] [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na Addaaramy]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipokuja Madina na watu wakamuona, haraka sana walimfuata, na miongo mwa waliomfuata ni Abdallah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake na alikuwa ni katika Mayahudi wakati huo, alipomuona akajua kuwa uso wake haukuwa wa mtu muongo; Kwa sababu ya kile kinachoonekana kwake kama, nuru, na uzuri, na heshima na ukweli, ikawa jambo la kwanza alilolisikia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwataka watu wafanye matendo yatakayopelekea kuingia Peponi, ikiwemo: La kwanza: kusambaza salamu ya amani, na kuionyesha na kuikithirisha kwa wale unaowajua na usiowajua. La pili: Kulishiza chakula kwa sadaka na zawadi na kukaribisha ugeni. La tatu: Kuunga udugu kwa wale kinachowaunganisha kizazi au ukaribu wa udugu upande wa baba au mama. La nne: Swala za sunna, kisimamo cha usiku na watu wakiwa wamelala.

فوائد الحديث

Ni sunna kueneza salamu ya amani baina ya Waislamu ama kwa asiye Muislamu haanzwi kwa salamu, na akimtolea salamu kwa kusema: Amani iwe juu yako, (Assalaam alaikum) amjibu kwa kusema: Na juu yako (Wa alaikum).

التصنيفات

Kisimamo cha Usiku., Ubora na fadhila za matendo mema.