Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili

Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili

Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".

[Sahihi] [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kubeba wajibu ni lazima kwa mwanadam isipokuwa hawa watatu: Mtoto mdogo mpaka akue na abalehe. Na kwa mwendawazimu aliyepoteza akili mpaka akili irudi. Na kwa aliyelala mpaka aamke. Kubeba wajibu kumeondolewa kwao, na kutenda kwao madhambi hakuandikwi, lakini mtoto huandikiwa kheri anapofanya, isipokuwa mwendawazimu na aliyelala; kwa sababu wote hawa wako katika kundi la mtu asiyekubalika ibada yake kwa kupoteza hisia.

فوائد الحديث

Kupoteza uwezo wa mtu hutokea ima kwa sababu ya usingizi, ambao unamzuia kuwa na uwezo wa kuwa macho ili kutekeleza wajibu wake, au kwa sababu ya umri wake mdogo na utoto, ambao unamfanya kupoteza uwezo, au kwa sababu ya wendawazimu ambao huvuruga kazi za akili yake, au kinachofananishwa na hayo kama vile ulevi, atakayepoteza uwezo sahihi wa kupambanua na kufikiri, akakosa sifa kwa sababu ya sababu hizi tatu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa uadilifu Wake na upole wake na ukarimu Wake amemuondolea dhambi kwa yale yanayotokea kwa makusudi au uzembe katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kutoandika dhambi zao hakufuti baadhi ya hukumu za kidunia dhidi yao; kama mwendawazimu akiua, hakuna kisasi wala kafara kwake, na mtu wake mwenye akili timamu lazima alipe fidia.

Kubalehe kuna dalili tatu: Kutokwa na manii, kwa kujiotea au kwa kinginecho, au kuota nywele sehemu za siri, au kutimiza miaka kumi na tano, na linaongezeka jambo la nne kwa mwanamke: nalo ni hedhi.

Amesema Al-Subki: Mtoto kijana, na wengine wakasema: Mtoto aliye tumboni mwa mama yake anaitwa kijusi, akizaliwa anaitwa mvulana, na akiachishwa kunyonya, basi ni mvulana mpaka saba, basi anakuwa kijana mpaka kumi, kisha mdogo hadi kumi na tano, na kilicho yakini ni kwamba anaitwa mvulana katika matukio yote haya, alisema Al-Suyuti.

التصنيفات

Masharti ya Swala.