Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema: Sami'allaahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) alikuwa hanyanyui yeyote miongoni mwetu mgongo wake mpaka aporomoke Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusujudu, kisha nasi tunaporomoka baada yake

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema: Sami'allaahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) alikuwa hanyanyui yeyote miongoni mwetu mgongo wake mpaka aporomoke Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusujudu, kisha nasi tunaporomoka baada yake

Kutoka kwa Abdallah bin Yazidi Al-Khatmiy amesema: Alinisimulia Al-Baraa naye si mtu wa kukadhibishwa, akasema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema: Sami'allaahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) alikuwa hanyanyui yeyote miongoni mwetu mgongo wake mpaka aporomoke Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusujudu, kisha nasi tunaporomoka baada yake.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Baraa bin Azibi radhi za Allah ziwe juu yake naye ni mkweli, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anasema: Sami'allahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi), walikuwa wakiendelea kusimama walioko nyuma yake, na hainamishi yeyote miongoni mwao mgongo wake kwa ajili ya kusujudu mpaka aweke rehema na amani ziwe juu yake paji lake la uso katika Ardhi, kisha wanaporomoka wote kwa kusujudu baada yake.

فوائد الحديث

Namna Maswahaba walivyomfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala, nakwamba wao walikuwa hawahami kutoka waliposimama kwenda katika sijida mpaka asujudu.

Amesema Bin Daqiiq Al-Idd: Katika hilo kuna ushahidi wa utulivu wa muda mrefu kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Maamuma kwa imamu wake ana hali nne katika kumfuata: 1- Kumtangulia: Kwa kuanza kitendo kabla ya imamu wake, kwa kufika maamuma katika rukuu kabla ya imamu hajafika, mfano: Kama akirukuu kabla ya imamu, au akasujudu kabla ya imamu, na hii ni haramu, na akikusudia kumtangulia huku akijua kuwa imekatazwa kufanya hivyo basi swala yake inaharibika, sawa awe kamtangulia kutoka katika nguzo au kwenda katika nguzo, na ikiwa ni katika takbira ya kuanza swala (ile ya kuhirimia swala) basi swala yake haitokubalika, na itamlazimu arudie upya swala yake. 2- Kwenda naye sawa, aende sawa na imamu, arukuu pamoja na rukuu yake na asujudu na sijida yake, na anyanyuke pamoja na kunyanyuka kwake, na kitendo hiki kwa uchache kabisa ni machukizo, na uwazi wa dalili unaonyesha kuwa ni haramu pia; na akienda sawa na imamu katika takbira ya kuanza swala, swala yake haitokubalika na atalazimika kurudia swala yake. 3- Kumfuata: Kwa kuleta vitendo vya swala baada ya imamu wake, pasina kuchelewa, na hii ndio namna bora na ya kisheria. 4- Kwenda kinyume naye, kwa kwenda kinyume na imamu wake kiasi ambacho kinamtoa katika kumfuata, kama imamu kurukuu na akabakia maamuma kasimama mpaka imamu akakaribia kunyanyuka kutoka katika rukuu, na hii ni kinyume na sheria na ni haramu, isipokuwa ikiwa ni kwa sababu ya maradhi au utu uzima.

التصنيفات

Hukumu ya Imamu na Maamuma.