Je mnajua ni nani aliyefilisika?

Je mnajua ni nani aliyefilisika?

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Je mnajua ni nani aliyefilisika?" Wakasema: Aliyefilisika kwetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yule asiye na Dirham (pesa) wala mali yoyote. Akasema: "Hakika aliyefilisika katika umma wangu ni yule atakayekuja siku ya Kiyama akiwa na (ibada za) swaumu na swala na zaka, na akaja akiwa kamtukana huyu, na kamzulia machafu huyu, na kala mali ya huyu, na amemwaga damu ya huyu na amempiga huyu, hivyo atapunguziwa huyu kutoka katika mema yake, na huyu katika mema yake, yakimalizika mema yake kabla hajamaliza kulipa anayodaiwa yatachukuliwa kutoka katika makosa yao yatatupwa kwake kisha atatupwa katika moto".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwauliza Maswahaba zake: Je, mnamjua aliyefilisika? Wakasema: Aliyefilisika miongoni mwetu ni yule asiye na fedha wala mali. Akasema: Aliyefilisika katika umma wangu Siku ya Kiyama ni yule anayefanya mambo mema kama Swala, Saumu na Zaka, na akaja akiwa kamshutumu huyu na kamtukana huyu, na kamsingizia mabaya mtu huyu katika heshima yake, na kala mali ya huyu na akakana, na akamwaga damu ya huyu na kumdhulumu, na kampiga huyu na akamdhalilisha, hivyo mtu aliyedhulumiwa atapewa kutoka katika matendo yake mema, mema yake yakimalizika kabla ya haki za watu na dhulma hazijamalizika, yatachukuliwa madhambi ya wale aliowadhulumu na kuwekwa katika vitabu vya dhalimu, kisha atatupwa na kurushwa motoni kwani hajabaki na jema.

فوائد الحديث

Tahadhari dhidi ya kutumbukia katika makatazo, hasa kuhusu haki za watu zenye kuonekana na zisizoonekana.

Haki za viumbe wao kwa wao mfumo wake ni kutosameheana, na haki za Muumba isipokuwa ushirikina, zimejengeka katika msamaha.

Kutumia njia ya mazungumzo ambayo humtia shauku msikilizaji, huvuta fikira zake, na huamsha hamasa yake, hasa katika elimu malezi na muongozo.

Kumeelezwa maana halisi ya mtu aliyefilisika, naye ni yule waliyechukua wadai wake amali zake njema Siku ya Kiyama.

Kisasi Akhera kinaweza kuja katika mema yote, kiasi kwamba kusibakie jema lolote.

Muamala wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake umesimama katika msingi wa uadilifu na haki.

التصنيفات

Maisha ya Akhera., Tabia mbovu.