إعدادات العرض
Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake
Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake
Kutoka kwa Abuu Shuraihi radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake".
[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
الشرح
Aliapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akasisitiza kiapo chake mara tatu, akasema: Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Maswahaba wakamuuliza: Na ni nani ambaye hawezi kuamini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ambaye jirani anahofia usaliti wake na dhulma zake na shari zake.فوائد الحديث
Kukanushwa imani kwa yule ambaye jirani yake hapati amani kutokana na dhulma zake na shari zake hili linaonyesha kuwa ni katika madhambi makubwa, na kwamba mfanyaji wake anaupungufu wa imani.
Himizo la msisitizo juu ya kumtendea wema jirani na kuacha kumuudhi kwa kauli au kitendo.
التصنيفات
Suluhisho na hukumu za ujirani.