إعدادات العرض
Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipokuwa muwe mnalia
Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipokuwa muwe mnalia
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Tulipita tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hijiri (miji ya Thamudi), akasema kutuambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipokuwa muwe mnalia; kwa kutahadhari msijekupatwa na mfano wa yale yaliyowapata" Kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mwendo mpaka akapapita.
الترجمة
العربية Tiếng Việt Bahasa Indonesia Nederlands English অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Hausa Românăالشرح
Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipopita katika miji ya Thamudi, kutoingia katika miji ya walioadhibiwa, wale waliozidhulumu nafsi zao au kuiendea miji hiyo, isipokuwa anayeingia kama atakuwa analia kwa kuchukua mazingatio kwao; kwa kuhofia asijekufikwa na mfano wa yale yaliyowafika miongoni mwa adhabu, kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mbio mpaka akaivuka.فوائد الحديث
Kutafakari katika hali za wale aliowaangamiza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuchukua tahadhari katika yale waliyotumbukia kwayo; na kuchukua tahadhari ya kujisahau kutozingatia alama.
Miji ya hao walioadhibiwa haitakiwi kuishi baada yao, na wala haifanwyi kuwa makazi, kwa sababu atakayeishi hapo hawezi kulia daima, na ilikatazwa kuingia ila kwa sifa hii.
Amesema Nawawi: Hapa kuna himizo la kuchunga wakati wa kupita katika miji ya madhalimu, na sehemu za adhabu, na mfano wake vile vile ni kwenda haraka katika bonde la Muhassiri (Liko Makkah, katika Mina na Muzdalifa); kwa sababu watu wa ndovu waliangamia huko, inatakiwa kwa mwenye kupita katika mfano wa sehemu hizi kuchunga na kuwa na hofu na kulia, na kuchukua mazingatio kwao na maangamizo yao, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hilo.
Katazo na tahadhari yanakusanya nyumba za Thamudi na wengineo wenye kufanana nao katika umma nyinginezo walioteremkiwa na adhabu.
Katazo la kuzifanya sehemu na maeneo haya kuwa sehemu za utalii na matembezi na mfano wake.
التصنيفات
Adabu na Hukumu za Safari.