إعدادات العرض
Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja
Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja
Kutoka kwa Hudhaifa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Watu wakasema: Sisi tulimsikia, akasema: Huenda nyinyi mnakusudia fitina ya mtu kwa familia yake na jirani yake? Wakasema: Ndivyo, akasema: Fitina hiyo inafutwa na swala na swaumu na sadaka, lakini ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza fitina ambayo inapiga kama mawimbi ya Bahari? Akasema Hudhaifa: Akawanyamazisha watu wote kwa hilo, nikasema: Mimi, akasema: Nakuapiza kwa Mwenyezi Mungu, umkose baba yako, ni wewe kweli, Hudhaifa, nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja, moyo wowote utakaozifyonza basi hutiwa ndani yake doa jeusi, na moyo wowote unaozikataa hutiwa doa jeupe, moyo huo mpaka unakuwa katika (hadhi ya) mioyo miwili, katika weupe mfano wa jiwe jeupe, hivyo hakuna fitina yoyote inayoweza kuudhuru milele kwa muda wote mbingu na ardhi zitakapoendelea kubakia kwake, na moyo mwingine ni mweusi ti! kama chungu kilichofunikwa, haukubali jema, wala haukatai ovu, isipokuwa matamanio ulionyweshwa", Hudhaifa akasema: Na nikamsimulia kuwa hakika kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa, na hivi karibuni utavunjwa, Omari akasema: Hivi utavunjwa? umepata hasara ya kumkosa baba, na lau ungelifunguliwa basi huenda ungelirejeshwa tena, nikasema: Hapana, bali utavunjwa, na nikamsimulia kuwa mlango huo ni mtu atauawa au kufa, na ni mazungumzo ya kweli wala si maneno ya kubumba. Akasema Abuu Khalidi, nikasema kumwambia Saa'di: Ewe Abuu Maaliki nini maana ya nyeusi ti!? Akasema: Ni weupe ung'aao katika weusi, anasema, nikasema: Na nini maana ya chungu kilichofunikwa? Akasema: Kilichogeuzwa juu chini.
الترجمة
العربية Tiếng Việt Bahasa Indonesia Nederlands English অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Hausa Românăالشرح
Alikuwa kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika kikao chake akiwa pamoja na kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, akasema kuwaambia: Ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume rehema na amni ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Wakasema baadhi yao: Sisi tulimsikia akieleza kuhusu fitina, akasema Omari radhi za Allah ziwe juu yake: Huenda nyinyi mnakusudia fitina na mtihani wa mtu katika mambo yake maalumu; kwa mke wake na mtoto wake, kwa kuchupa mipaka katika kuwapenda, na pupa yake kwao, na kushughulishwa nao sana kuliko mambo ya kheri, au kwa uzembe wake, kwa kutotekeleza mambo ya lazima kwake kuyasimamia katika haki, na kuwaadabisha na kuwasomesha, na vile vile fitina ya mtu kwa jirani yake na mfano wake, huenda nyinyi mnakusudia hiyo? Wakasema: Ndiyo, akasema: Hiyo ni fitina inayopelekea kuihesabu nafsi, ikiwa ni pamoja na madhambi ambayo yanatarajiwa kufutwa kwa mema, kama swala na swaumu na sadaka. Lakini ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiitaja fitina inayowakumba watu wote kwa sababu ya ukubwa wake na wingi wa kusambaa kwake, inayowavuruga watu kama yanavyovurugika mawimbi ya Bahari? Watu wote wakanyamaza: Akasema Hudhaifa bin Yamani radhi za Allah ziwe juu yake: Mimi nilimsikia, Omari radhi za Allah ziwe juu yake akafurahi, na akasema kumwambia: Umenishangaza kwa haya aliyokuja nayo mtu mfano wako!: Basi hebu sema: Hudhaifa akasema: Amesema rehema na amani ziwe juu yake: Fitina itatokea na itafungamana na mwili na upande wa moyo wa mtu kama godoro linavyonasa udongo katika mbavu za aliyelala hapo, na zitamuathiri katika moyo kwa kushikamana nazo sana, na kutoziacha fitina hizi, na kujirejea rejea kwake fitina baada ya fitina, moyo wowote utakaoingia ndani yake, na ukazipenda, na zikachanganyika nao, kama kuchanganyikana na kinywaji na kuingia ndani yake; basi litapigwa ndani ya moyo wake doa jeusi; na moyo wowote utakaozikataa, basi utapigwa ndani yake doa jeupe, mpaka nyoyo zitakuwa katika aina mbili; katika moyo mweupe kwa sababu ya kushikamana na imani kisawasawa, na kusalimika kwake na mapungufu, na kwamba fitina haijaambatana nao, na wala hazijauathiri mfano wa jiwe gumu jeupe ambalo hakuna kitu kinaweza kunasa hapo, hakuna fitina inayoweza kumdhuru mpaka mtu atakapokutana na Mwenyezi Mungu. Na moyo mwingine ni moyo uliobadilika rangi yake na kuwa mweusi kwa sababu ya fitina, ni kama birika lililolala upande, au lililogeuzwa ambalo hakuna maji yanayoweza kutulizana ndani yake, basi vile vile moyo huu hakuna kheri wala hekima yoyote inayoweza kunasa ndani yake, haukubali jema, na wala haukatai baya, isipokuwa yale aliyoyapenda, na nafsi yake kuegemea kwayo. Na akasema Hudhaifa kumwambia Omari: Hakika fitina hiyo hakuna chochote kitakachotokea katika zama za uhai wako, lakini kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa na unakaribia kuvunjwa, akasema: Yaani utavunjwa kwa nguvu? na lau kama ungelifunguliwa basi ungelirejeshewa ukafungwa tena, akasema Hudhaifa: Hapana, bali utavunjwa, na kwamba mlango huo ni mtu atauawa au atakufa. Na niliyoyaeleza ni habari za kweli na si katika habari za Mayahudi na Wakristo, na wala si jitihada za mtu mwenye mtazamo wa mbali, bali ni katika hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.فوائد الحديث
Hatari ya fitina ya watu wote; kwa sababu ya yale yanayotokea ndani yake kama umwagwaji wa damu na kupoteza mali na kutoweka kwa amani.
Fitina binafsi ikiwa inahusiana na dini basi hapa mtu kasemwa vibaya; kwa sababu ima iwe ni uzushi au maasi, na ikiwa inafungamana na mambo ya kidunia, basi huu kwake ni mtihani, na la wajibu kwake ni kuwa subira.
Moyo unaathirika kwa fitina zinazopitishwa, na mwenye kuwezeshwa ni yule aliyeongozwa na Mwenyezi Mungu kudumu katika uongofu.
Amesema Nawawi: Amesema Mtunzi wa kitabu Attahriiri: Maana ya hadithi: Nikuwa mtu atakapofuata matamanio yake na akafanya maasi, moyo wake huingia giza kwa kila maasi anayoyafanya, na akiendelea hivyo basi hufitinika na kuondoka nuru ya Uislamu, na moyo kuwa kama mfano wa chungu kikijifunika humwagika kilichomo, na hakiwezi kuingia kitu tena baada ya hapo.
Kauli ya Omari kwa Hudhaifa: (Umkose baba yake) Maana yake: Umedhamiria kweli katika jambo hili, na kaza na ujiandae kujiandaa kwa mtu asiyekuwa na msaidizi.
Ubora wa Omari radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mlango uliofungwa baina ya watu na fitina