Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo

Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika, mwenye kiwango cha chini zaidi kati yenu katika Pepo ni kwamba ataambiwa: "Tamani!" Basi atatamani na atamani, na ataambiwa: "Je umeshatamani?" Atasema: "Nidyo." Ataambiwa: "Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye nafasi na daraja ndogo zaidi kwa wale watakaoingia peponi, ataambiwa: Tamani, basi atatamani, na atatamani tena, mpaka atafikia mahali ataishiwa yote ya kutamani isipokuwa atayataja, hapo ataambiwa: Je, umetamani umefika mwisho? Atasema: Ndiyo, hapo ataambiwa: Basi ni vyako vyote ulivyotamani na mfano wake pamoja navyo.

فوائد الحديث

Kutofautiana kwa nafasi za watu wa peponi.

Kumebainishwa ukubwa wa karama ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Neema za peponi hazishii katika kitu maalumu, bali muumini atapata ndani yake kila anachokitamani na nafsi yake kuwa na hamu nacho, ikiwa ni fadhila na ukwasi na ukarimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التصنيفات

Maisha ya Akhera., Sifa za pepo na moto.