Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini…

Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala ya Idil Adhaa au Fitri kwenda katika uwanja wa kuswali, akapita kwa wanawake, akasema: "Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi", Wakasema: Na ni upi upungufu wa dini yetu na akili zetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hivi kwani si ushahidi wa mwanamke mmoja ni sawa na ushahidi nusu wa mwanaume?" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Hilo ni katika upungufu wa akili yake, na je hivi akiingia katika hedhi si haswali wala hafungi" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Basi hilo ni katika upungufu wa dini yake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika siku ya Iddi kwenda katika uwanja wa swala, na alikuwa kawaahidi wanawake kuwa atawatengea nafasi ya kuwapa mawaidha, akaitimiza siku hizo, na akasema: Enyi kundi la wanawake toeni sadaka, na zidishe kuomba msamaha; kwani mambo mawili hayo ni katika sababu kubwa za kufutiwa madhambi, kwani mimi nilikuoneni usiku niliopandishwa mbinguni mkiwa wengi motoni. Mwanamke mmoja miongoni mwao mwenye akili na mawazo mazuri na heshima, akasema: Kwani tuna nini sisi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mpaka tuwe wengi motoni? Akasema: Kwa sababu ya mambo kadhaa: Mnazidisha sana kulaani na matusi, na mnakanusha haki za waume. Kisha akawasifu kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: Sijapata kuona wenye mapungufu ya akili na dini wanaoweza kuwashinda wenye mioyo salama na akili na maamuzi na uwezo wa kutunza kumbukumbu zao kuliko nyinyi. Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni upi upungufu wa akili na dini? Akasema: Ama upungufu wa akili ni kuwa ushahidi wa wanawake wawili unalingana na ushahidi wa mwanaume mmoja; huu ndio upungufu wa akili, na upungufu wa dini, ni upungufu wa kufanya amali njema, kiasi ambacho mwanamke anakaa siku kadhaa haswali kwa sababu ya hedhi, na anafungua siku kadhaa za Ramadhani kwa sababu ya hedhi, na huu ndio upungufu wa dini, isipokuwa wao hawalaumiwi wala hawaandikiwi dhambi juu ya hilo; kwa sababu ni katika asili ya maumbile, kama ambavyo mwanadamu ameumbwa na asili ya kuipenda mali, na haraka katika mambo yake na ni mjinga.... na mengineyo, lakini alilitanabahisha hilo ikiwa ni tahadhari kwa wanaume wasifitinike nao.

فوائد الحديث

Sunna kwa wanawake kutoka kwenda katika swala ya Iddi, na watengewe muda wa mawaidha.

Kuwapinga waume na kukithirisha laana ni katika madhambi makubwa; kwa sababu kuahidiwa moto ni katika alama za dhambi kuwa katika madhambi makubwa.

Hapa kumebainishwa kuzidi kwa imani na kupungua kwake, yatakayekithiri matendo yake, basi imani yake na dini yake vitazidi, na zitakayepungua ibada zake dini yake itapungua.

Amesema Imam Nawawi: Akili inakubali kuzidi na kupungua, na vile vile imani, na si makusudio ya kutajwa mapungufu kwa wanawake ni kuwalaumu kwa hilo; kwa sababu hilo ni katika asili ya maumbile, lakini tanbihi katika hilo ni kutahadharisha kutofitinika nao, na ndio maana amepanga adhabu kwa yale yaliyotajwa ikiwemo kuwapinga waume na mengineyo na si katika mapungufu, na mapungufu ya dini hayaishii tu katika madhambi bali ni zaidi ya hayo.

Hapa kuna swala la mwanafunzi kumrejea mwalimu, na mfuasi kumrejea anayemfuata katika yale ambayo kwake maana haijawa wazi.

Ndani ya hadithi kumeelezwa kuwa ushahidi wa mwanamke mmoja ni nusu ya ushahidi wa mwanaume mmoja, na hii ni kwa sababu ya upungufu wa kumbukumbu zake.

Amesema bin Hajari katika kauli yake: "Sijapata kuona wapungufu...mpaka mwisho" Kinachodhihiri kwangu nikuwa, hili ni miongoni mwa sababu za kuwa kwao wengi motoni; kwa sababu wao wakiwa sababu ya kuondoa akili ya mwanaume shupavu mpaka akafikia kufanya au kusema maneno yasiyofaa watakuwa wameshirikiana naye katika madhambi na tena wamemzidi.

Uharamu wa swala na swaumu kwa mwanamke wakati wa hedhi yake, na mfano huo huo kwa mwenye nifasi, kisha watalipa swaumu pekee watakapokuwa twahara.

Uzuri wa tabia ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani aliwajibu wanawake maswali yao pasina ukali wala kuwalaumu.

Amesema bin Hajari: Nikuwa sadaka inazuia adhabu, nakuwa inafuta makosa yaliyoko baina ya viumbe.

Amesema Nawawi: Upungufu wa dini kwa wanawake kwa sababu ya kuacha kwao swala na swaumu katika wakati wa hedhi; kwa sababu zitakayekithiri ibada zake basi itaongezeka imani yake na dini yake, na zitakayepungua ibada zake itapungua dini yake, kisha upungufu wa dini unaweza kuwa katika sura ambayo anapata dhambi, kama atakayeacha swala au swaumu au mengineyo katika ibada za wajibu juu yake pasina udhuru, na inaweza kuwa katika sura ambayo hapati madhambi, kama atakayeacha swala ya Ijumaa au kwenda vitani au mengineyo ambayo si wajibu juu yake pasina udhuru, na inaweza kuwa katika sura ambayo yeye ndiye kalazimishwa kwa hilo, kama mwenye hedhi kuacha swala na swaumu.

التصنيفات

Hukumu za wanawake., Sifa za pepo na moto.