Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne baada yake basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni

Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne baada yake basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni

Kutoka kwa Ummu Habiba, radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne baada yake basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni".

[Sahihi]

الشرح

Amempa habari njema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake atakayeswali katika swala za sunna rakaa nne kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa nne baada yake, na akadumu na akazihifadhi, kuwa Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni.

فوائد الحديث

Ni sunna kuhifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na nne baada yake.

Sunna zilizopangwa za kabla ya swala - Yaani kabla ya swala za faradhi-; zina hekima kubwa, miongoni mwake: Ni kumuandaa mwenye kuswali kwa ajili ya ibada kabla ya kuingia katika swala ya faradhi, na ama za baada ya swala miongoni mwa hekima zake ni kuziba mapungufu ya swala za faradhi.

Sunna zilizopangiliwa zina faida kubwa, ikiwemo kuzidisha mema, na kufuta madhambi, na kunyanyua daraja.

Kanuni ya Ahlussunna (wanaofuata mafundisho ya Mtume) katika hadithi za ahadi mfano wa hadithi hii: Ni kuchukuliwa kuwa, mpaka mtu afe katika hali ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, nakuwa makusudio yake ni kutokaa milele motoni, kwa sababu mfanya madhambi ni katika watu wa tauhidi, anastahiki adhabu lakini hatowekwa motoni milele endapo ataadhibiwa.

التصنيفات

Sunna za kila siki zilizopangiliwa