Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu

Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kupigwa mtu yeyote zaidi ya viboko kumi isipokuwa katika maasi, na pia hakuna maelekezo yoyote yaliyokuja katika sheria kueleza idadi maalumu ya viboko au kipigo au adhabu maalumu, na makusudio yake haizidishwi katika kipigo cha kuadabisha zaidi ya viboko kumi, kama kumpiga mke au mtoto.

فوائد الحديث

Mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyoiamrisha au aliyoikataza inaadhabu zinazokomesha hayo, ima zimepangwa katika sheria, au zinarudi kukadiriwa kwake katika masilahi anayoyaona hakimu.

Kutia adabu kunakuwa kwa kiasi kidogo, kwa kiasi cha kuelekeza na kuhofisha, kusizidishwe zaidi ya viboko kumi ikibidi kufanya hivyo, na kilichobora zaidi ni kuwaadabisha pasina kuwapiga, bali kwa kuwaelekeza, na kuwafundisha, na kuwaongoza, na kuwatia hamasa, hilo huleta msukumo mkubwa wa kukubali na upole katika kujifunza, na hali katika nafasi hii hutofautiana sana, inapasa mtu afanye kinachofaa.

التصنيفات

Hukumu za uaibishaji.