إعدادات العرض
Atakayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au wa mifugo, basi yatapungua katika matendo yake kila siku kiratu (shehena) mbili
Atakayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au wa mifugo, basi yatapungua katika matendo yake kila siku kiratu (shehena) mbili
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au wa mifugo, basi yatapungua katika matendo yake kila siku kiratu (shehena) mbili", Amesema Salim: Na alikuwa Abuu Huraira akisema: "Au mbwa wa shamba", Naye akawa na shamba.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français ئۇيغۇرچە Hausa Português മലയാളം Kurdî Русский Tiếng Việt অসমীয়া Nederlands አማርኛ ગુજરાતી සිංහල ไทยالشرح
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufuga mbwa, isipokuwa kwa haja ya kuwinda, au kulinda mifugo na mazao, na atakayemfuga pasina haja hizo zitapungua katika thawabu za matendo yake kila siku shehena mbili; ambazo ujazo wake unajulikana mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.فوائد الحديث
Hifai kwa muislamu kufuga mbwa, isipokuwa katika hali zilizotajwa.
Kukatazwa kufuga mbwa; kwa sababu ya hasara na madhara mengi yanayopatikana ndani yake, kwani imethibiti kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hawaingii nyumba ambayo kuna mbwa ndani yake; na ni kwa sababu mbwa ananajisi nzito ambayo hakuna kinachoweza kuiondosha isipokuwa kurudiarudia kuosha kwa maji na udongo.
التصنيفات
Uwindaji