Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru

Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Katada -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ndoto nzuri yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mtu kuota anayoyachukia na kumhuzunisha hutoka kwa Shetani. Atakayeota yanayomchukiza basi ateme kushotoni kwake, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake; kwani haitomdhuru, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu amefanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na hayo yenye kuchukiza yanayoambatana na ndoto.

فوائد الحديث

Ndoto nzuri na mbaya ni yale mambo anayoyaona mtu aliyelala, lakini ndoto nzuri nyingi ni zile anazoota mtu katika mambo ya kheri au mambo mazuri, na ndoto nyingi mbaya huwa katika yale anayoyaona mtu katika mambo ya shari na mabaya, kila moja kati ya hayo hukaa mahala pa lingine.

Migawanyiko ya ndoto: 1- Ndoto njema, nayo ni ndoto ya kweli na ni bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu anayoiona au ikaonwa na mtu mwingine kwake, 2- Mazungumzo ya nafsi, nayo ni yale ambayo mtu huzungumza na nafsi yake akiwa macho (kisha yanajirudia akiwa usingizini), 3- Huzuni na hofu ya Shetani na vitisho vyake ili tu amhuzunishe mwanadamu.

Jambo la msingi katika mambo yaliyotajwa katika milango ya ndoto ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo, na ajipe bishara njema kwayo, na aihadithie lakini kwa yule anayempenda na si kwa anayemchukia.

Na la msingi katika yale yaliyotajwa katika adabu za ndoto mbaya ni mambo matano: Ajilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme pale tu anashituka kutoka usingizini upande wa kushoto mara tatu, na kamwe asiisimulie kwa yeyote, na akitaka kurudi katika usingizi wake basi abadili ubavu aliokuwa awali; kwani ndoto hiyo haitomdhuru.

التصنيفات

Adabu ya kuona Ndoto