Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala

Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala, pindi anapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu linafunguka fundo moja, akitawadha, linafunguka fundo jingine, na akiswali, yanafunguka mafundo yake yote, anaamka akiwa na uchangamfu na moyo mkunjufu, na vinginevyo basi anaamka akiwa na nafsi chafu tena mvivu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya shetani na mapambano yake na mwanadam anayetaka kusimama kwa ajili ya swala ya usiku au Alfajiri. Muumini anapokwenda kulala shetani hufunga katika kisogo chake -yaani mwisho wa kichwa chake- mafundo matatu. Muumini atakapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akawa hajatii wasi wasi wa shetani; fundo moja hufunguka. Akitawadha linafunguka fundo jingine. ..... Na ikiwa atasimama akaswali yatafunguka mafundo yote matatu, na atakuwa na uchangamfu wa nafsi; na kufurahi kwake kwa yale aliyoafikishwa na Mwenyezi Mungu katika ibada, akijipa bishara kwa yale aliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu katika thawabu na msamaha, ikiwa ni pamoja na hivyo vilivyomuondokea katika mafundo ya shetani na vikwazo vyake, na asipofanya hivyo atakuwa na nafsi chafu, atakuwa na moyo wenye huzuni, mvivu katika mambo ya kheri na mambo mema; kwa sababu atakuwa kafungwa kwa pingu za shetani, na atakuwa kawekwa mbali na kumkaribia Rahmani (Mwingi wa rehema).

فوائد الحديث

Shetani siku zote anakwenda mbio katika njia zote za mwanadam; ili azuie kati yake na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mja hawezi kusalimika na shetani isipokuwa kwa kutaka msaada kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kuchukua sababu za kinga na ulinzi.

Kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kunaleta uchangamfu katika nafsi na kunakunjua kifua, na hufukuza uvivu na kupoa, na huondoa matatizo na hasira; kwa sababu humfukuza shetani, na hili ni katika wasi wasi wake.

Muumini hufurahishwa na taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutekeleza ibada zake, na anasononeka kwa uzembe wake katika kupunguza daraja za fadhila na ukamilifu.

Kujisahahu na kukaa katika maasi ni katika matendo ya shetani na kupambia kwake.

Mambo haya matatu -Kumtaja Mwenyezi Mungu, na udhu, na swala- humfukuza shetani.

Shetani kufunga mwisho wa kichwa pekee; ni kwa sababu ndio kituo cha nguvu, na ndio sehemu ya kutolea maamuzi, akifunga mahali hapo huweza kuitawala roho ya mwanadam, na kumtia usingizi.

Amesema Imam bin Hajari Al-Asqalaani: Umetajwa usiku katika kauli yake: "Tumia usiku huu" Inaonyesha hili ni maalumu kwa usingizi wa usiku.

Amesema bin Hajar Al-Asqalani: Hakuna dhikri makhsusi ambayo haitoshelezi nyingine, bali kila kinachofaa kuitwa dhikri kinatosheleza, na inaingia ndani yake kusoma Qur'ani, kusoma hadithi za Mtume, na kujishughulisha na kusoma elimu ya Kisheria, na jambo bora zaidi lililotajwa ni kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Atakayeshituka usiku kutoka usingizini akasema: "Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye juu ya kila kitu ni muweza, kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, na ametakasika Mwenyezi Mungu, na hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Mkubwa, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha akasema: Ewe Mola wangu, nisamehe, au akiomba dua yake itaitikiwa, na akitawadha utakubaliwa udhu wake" Kaipokea Bukhari.

التصنيفات

Fadhila - ubora wa kutawadha., Faida za Kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.