إعدادات العرض
Msaidie ndugu yako akiwa amedhulumu au kudhulumiwa
Msaidie ndugu yako akiwa amedhulumu au kudhulumiwa
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Msaidie ndugu yako akiwa amedhulumu au kudhulumiwa", Akasema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unaonaje ikiwa ndugu yangu kadhulumu, vipi nitamsaidia? Akasema: "Unamuhama au unamzuia asifanye dhulma, kwa kufanya hivyo ndiyo kumnusuru".
[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Românăالشرح
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha Muislamu kumsadia ndugu yake Muislamu sawa sawa awe kadhulumu au kadhulumiwa, mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimnusuru atakapokuwa emedhulumiwa kwa kumuondolea dhuluma, wasemaje ikiwa kadhulumu nitamsaidia vipi? Akasema: Utamzuia, na kumshika mkono na umkinge na umzuie na dhuluma; kwa kufanya hivyo ndiko kumnusuru dhidi ya Shetani wake na nafsi yake yenye kuamrisha maovu.فوائد الحديث
Hapa kuna tahadhari juu ya haki miongoni mwa haki za udugu wa kiimani baina ya Waislamu.
Kumzuia dhalimu, na kumkataza dhidi ya dhuluma.
Uislamu unakwenda kinyume na uelewa wa zama za ujinga, kiasi ambacho walikuwa wakisaidizana sawa sawa wawe wamedhulumiwa wao wamemdhulumu mwingine.
التصنيفات
Jamii ya Kiislamu