Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri

Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri

Kutoka kwa Abuu Haazim amesema: Nilikaa karibu na Abuu Huraira kwa muda wa miaka hamsini, nikamsikia akihadithia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema: "Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri" Wakasema: Unatuamrisha nini? Akasema: "Timizeni ahadi ya utiifu ya moja baada ya nyingine, wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza walikuongozeni vipi".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa wana wa Israeli walikuwa wakiongozwa na Manabii, na wakisimamia mambo yao kama wanavyofanya viongozi na watawala kwa raia, kila unapodhihiri ufisadi Mwenyezi Mungu anawatumia Nabii kwa ajili ya kunyoosha mambo yao na kuondoa yale waliyoyabadilisha katika hukumu. Na hakika hakuna Nabii baada yangu ili afanye kama waliyokuwa wakiyafanya wale, na watakuja baada yangu watawala, na watakuwa wengi, na utatokea mzozano na kuhitilafiana baina yao. Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao wakamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Unatuamrisha tufanye nini? Akasema: Atakapochaguliwa kiongozi baada ya kiongozi; uteuzi wa kiongozi wa kwanza ndio uteuzi sahihi na ni wajibu kuutimiza na kuuheshimu, na uteuzi wa pili ni batili na ni haramu kwake kuukataa, na wapeni haki zao, na muwatii na muishi nao kwa usikivu na utii isipokuwa katika maasi, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza na atawahesabu kwa yale wanayokufanyieni.

فوائد الحديث

Nikuwa ni lazima kwa raia kuwa na nabii au kiongozi mwenye kusimamia mambo yao, na mwenye kuwapeleka katika njia iliyonyooka.

Nikuwa hakuna nabii baada ya Nabii wetu Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake.

Tahadhari ya kujitoa kwa yule ambaye umethibiti uongozi wake kwa njia ya kisheria.

Haifai kuweka makubaliano ya kuwachagua viongozi wawili kwa wakati mmoja.

Ukubwa wa majukumu ya uongozi, kwa sababu Mwenyezi Mungu atamuuliza kuhusu raia wake.

Amesema bin Hajari: Kutanguliza jambo la dini kuliko jambo la dunia; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliamrisha kutimiza haki ya kiongozi kwakuwa ndani yake kuna kuipa nguvu dini na kuzuia fitina na shari; na kuchelewesha swala kudai haki yake haina maana ya kuidondosha, na Mwenyezi Mungu alimuahidi kuwa yeye mwenyewe atamlipa na atamtimizia hata kama ni huko Akhera.

Alama miongoni mwa alama za unabii wake rehema na amani ziwe juu yake, hakika walikithiri viongozi baada yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umma ukaongozwa na waliokuja kutengeneza miongoni mwao na walioharibu.

التصنيفات

Visa na hali za Umma uliopita.