إعدادات العرض
Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka
Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Kurdî Tiếng Việt Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Hausa Românăالشرح
Amemfananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyesoma Qur'ani na akakizoea kisomo chake sawa iwe kwa kutazama katika msahafu au kuhifadhi kwa moyo, na mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa kwa kamba ambazo hufungiwa wanyama, akimtazama mara kwa mara ataendelea kumshika na kumzuia, na akiacha kumfunga na kumtazama basi ataondoka na kutoroka, akianza kusoma Qur'ani msomaji wa Qur'ani basi huikumbuka, na asipoisoma basi ataisahau; madam kudumu kuisoma kutaendelea basi hifdhi yake itaendelea kubakia.فوائد الحديث
Himizo la kushikamana na Qur'ani na kuisoma, na tahadhari ya kutumbukia katika kuisahau.
Kudumu kuisoma Qur'ani huudhalilisha ulimi na huurahisishia kuisoma kwake, akiihama inakuwa nzito kwake na inampa tabu.
Amesema Kadhi: Na maana ya "Mwenye Qur'ani" Yaani: Aliyeizoea, na kusuhubiana: Ni kuzoea, na hukusudiwa: Fulani ni jamaa wa fulani, na watu wa peponi na watu wa motoni.
Miongoni mwa njia za ufundishaji ni kupiga mifano.
Amesema bin Hajari: Na amemtaja ngamia pekee; kwa sababu ndio mnyama pekee anayetoroka haraka zaidi katika wanyama wafugwao na binadamu, na kumkamata kwake baada ya kutoroka ni kazi ngumu sana.