Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma

Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma".

[Sahihi]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ahadi kali ya adhabu kuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama mtazamo wa huruma mwanaume aliyemuingilia mwanaume mwenzake katika utupu wake wa nyuma, au mwanamke katika utupu wake wa nyuma, nakuwa hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.

فوائد الحديث

Mwanaume kumwendea mwanaume mwenzake (Ulawiti) ni katika madhambi makubwa.

Kumwendea mwanamke katika tupu yake ya nyuma ni katika madhambi makubwa.

"Hamtazami Mwenyezi Mungu" Yaani: Mtazamo wa huruma au upole, na si makusudio yake: Kutazama kwa ujumla; kwa sababu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka hakuna chochote kinachofichikana kwake na hakitoweki machoni mwake chochote.

Matendo haya ni katika machafu makubwa na ni hatari sana kwa binadamu; kwakuwa ndani yake kuna kwenda kinyume na maumbile salama ya kibinadamu, na kupungua kwa kizazi, na kuharibu maisha ya ndoa, na kupandikiza uadui na chuki, na kuingia katika maeneo machafu yenye kutia kinyaa.

التصنيفات

Hukumu za uaibishaji.