Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda

Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda".

[Sahihi]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekuwa na mke zaidi ya mmoja, akawa hakufanya uadilifu baina ya wake zake uadilifu unaowezekana, ikiwemo kuwafanyia usawa katika matumizi na makazi na mavazi na malazi, nikuwa adhabu yake siku ya Kiyama nusu ya mwili wake itakuwa imepinda, na kupinda kwake ni adhabu kwake kwa sababu ya dhulma yake, kama alivyopinda katika muamala wake.

فوائد الحديث

Uwajibu wa mgao kwa mwanaume baina ya wake zake, na ni haramu kwake kuegemea kwa mmoja wao na kuwaacha wengine, katika yale anayoyaweza miongoni mwa matumizi, na malazi, na kukutana nao kwa wema, na mfano wa hayo.

Kufanya usawa katika mgao na mfano wa hayo, katika yale anayoyamiliki mtu, ama yale asiyoyamiliki kama mapenzi na kuegemea kwa moyo, hayo hayaingii katika hadithi, na ndio yaliyokusudiwa katika kauli yake Mtukufu: "Na kwamwe hamtoweza kutenda uadilifu kati ya wanawake hata mkifanya pupa (juu ya hilo) [An-Nisaa: 129].

Malipo huendana na namna ya matendo, kwa sababu mwanaume alipoegemea upande mmoja duniani kwa mwanamke mmoja akamuacha mwingine, atakuja siku ya Kiyama moja kati pande zake ukiwa umepinda umepishana na mwingine.

Kuheshimu haki za waja, nakuwa haki hizo hazisameheki; kwa sababu zimejengeka katika uchoyo na kulipizana.

Inapendeza kuishia mke mmoja, mwanaume akihofia kutowatendea uadilifu wake zake; ili asiangukie katika madhaifu katika dini; amesema Mtukufu: "Ikiwa mtahofia kutowafanyia uadilifu basi (bakini na) mmoja" [An-Nisaa: 3].

التصنيفات

muamala wa wanyumba wawili.