Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu

Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu

Kutoka kwa Abuu Waaqidi All-laithi radhi za Allah ziwe juu yake. Yakuwa Mtume rehema na amani zimfikie alipotoka kwenda katika vita vya Hunaini alipita katika mti wa washirikina ukiitwa: Dhata anwatwi (Mahala pa kutundika silaha) wakitundika silaha zao hapo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tuwekee nasi mahala pa kutundikia kama ambavyo wao wana mahala pa kutundikia, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Sub-haanallaah (Ametakasika Mwenyezi Mungu)! Maneno haya ni kama yale waliyosema watu wa Mussa: "Tufanyie nasi mungu kama walivyo wao na mungu" [Al-A'raaf: 138] Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu".

[Sahihi]

الشرح

Alitoka Mtume rehema na amani zimfikie kwenda Hunaini: Nalo ni bonde liko kati Twaif na Makka, na walikuwa pamoja naye baadhi ya Masahaba waliokuwa hawana muda mrefu tangu kuingia ndani ya Uislamu, wakapita katika mti ukiitwa: "Dhaata anwaatwi", yaani: Wenye vifaa vya kutundikia, washirikina walikuwa wakiutukuza na wakitundika hapo silaha zao na vitu vingine kwa kutaka baraka, wakaomba kutoka kwa Mtume rehema na amani zimfikie awawekee mti mfano wake, wakitundika hapo silaha zao, kwa kutafuta baraka, kwa kudhani kwao kuwa jambo hilo linafaa, Mtume rehema na amani zimfikie akamtukuza Mwenyezi Mungu kwa kukemea kauli hiyo, na kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu, na akawaeleza kuwa kauli hii inafanana na kauli ya watu wa Mussa kwake: "Tuwekee nasi mungu kama ambavyo wao walivyo na mungu", walipowaona wenye kuabudu masanamu wakaomba nao wawe na masanamu kama washirikina walivyo na masanamu, nakuwa kitendo hiki ni katika kufuata njia yao, kisha akaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa Umma huu utafuata mfumo wa Mayahudi na Wakristo na utafanya vitendo vyao, na akatahadharisha hilo.

فوائد الحديث

Mwanadamu anaweza kuliona zuri jambo akidhani kuwa linamuweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, hali yakuwa linamtenga mbali naye.

Ni wajibu kwa Muislamu kumtukuza Mwenyezi Mungu (Kumsabihi) na kutoa takbira anaposikia maneno yasiyofaa kusemwa katika dini, na wakati wa kustaajabu.

Ni katika shirki kutaka baraka katika miti na mawe na vinginevyo, na baraka hazitafutwi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Sababu za kuabudu masanam ni kuyatukuza, na kukaa hapo, na kuyataka baraka.

Uwajibu wa kuziba milango na njia zinazopelekea katika ushirikina.

Dalili zilizokuja kuwasema kwa ubaya Mayahudi na Wakristo ni tahadhari kwetu.

Katazo la kujifananisha na watu wajinga na Mayahudi na Wakristo, isipokuwa katika yale ambayo dalili zimekuja kuwa ni katika dini yetu.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.