Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile

Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile

Imepokelewa kutoka kwa Matwar Bin Ukaamis -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu akimpangia mtu kuwa afie katika ardhi fulani na hali yakuwa yeye hayupo katika ardhi hiyo; Basi humfanya ahitajie kitu katika ardhi ile hivyo ataenda katika ardhi ile, basi huchukuliwa roho yake akiwa huko.

فوائد الحديث

Hadithi inathibitisha maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na nafsi haijui itafia katika ardhi gani."

التصنيفات

Ni kuamini hukumu na mipangilio, Mauti na Hukumu zake.