Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala

Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala

Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa maneno matano, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala, hushusha mizani ya uadilifu na huinyanyua, yanapandishwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, pazia lake ni nuru, -na katika riwaya nyingine-: Lau kama angeliondoa, basi utukufu wa uso wake ungeunguza viumbe vyake mpaka pale ambapo macho yake yanafikia."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alisimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubia kwa Maswahaba zake kwa sentensi tano kamilifu, nazo ni: Ya kwanza: Kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka halali. Ya pili: Haiwezekani katika haki yake kulala; kulingana na ukamilifu wa usimamizi wake na uhai wake. Ya tatu: Ya kwamba Yeye Mtukufu anashusha mizani na kuinyanyua kulingana na vile vinavyopimwa miongoni mwa matendo ya waja yanayopanda kwake juu, na zinapimwa riziki zao zinazoshuka katika Ardhi, riziki ambayo ndiyo sehemu na fungu la kila kiumbe huishusha Yeye Mtukufu na kumfanya awe masikini, na huipandisha na kumfanya awe tajiri. Ya nne: Hupandishwa kwake waliyoyafanya waja usiku kabla ya mchana unaofuata baada yake, na amali zao za mchana kabla ya amali za usiku unaofuata baada yake; Malaika wanaohifadhi matendo ya waja hupanda na matendo ya usiku baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa mchana, na wanapanda na amali za mchana baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa usiku. Ya tano: Pazia lake Mtukufu linalozuia kumuona ni nuru au moto, laiti angelifunua basi mwangaza wa uso wake ungeunguza kila kitu mpaka pale linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; mwangaza wa uso wake ni nuru yake na utukufu wake na mng'ao wake. Na makadirio: Nikuwa, lau angeliondoa na kukifunua kinachozuia kumuona ambacho ni pazia, na akajitokeza wazi nuru ya uso wake ingeliunguza kila kitu mpaka linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; navyo ni viumbe vyote; kwa sababu jicho lake Aliyetakasika na kutukuka limezingira viumbe vyote.

فوائد الحديث

Kumebainishwa kutowezekana kulala kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwakuwa hilo ni katika mapungufu, na yeye ametakasika na hayo.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anamtukuza amtakaye na anamdhalilisha amtakaye, na anamuongoza amtakaye na anampoteza amtakaye katika waja wake.

Matendo hunyanyuliwa kwa Mwenyezi Mungu kila mchana na usiku, na katika hilo kuna himizo kwa waja wamchunge Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka katika usiku wao na mchana wao.

Hadithi inaonyesha uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na uzuri wa upangiliaji wake wa mambo ya viumbe wake, na hakuna shaka kuwa hii ni katika sifa za ukamilifu wake Aliyetakasika na kuwa juu.

Kumethibitishwa pazia lake Aliyetakasika na kutukuka, nayo ni nuru inayokinga baina yake na baina ya viumbe wake, na lau isingekuwa hiyo wanageliungua.

Amesema Aajurri: Hakika watu wa haki humsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kile alichojisifu mwenye Mtukufu, na kwa kile alichomsifu nacho Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na kwa kile walichomsifia Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na huu ndio msimamo wa wanachuoni katika wale walioamua kufuata sheria na hawakuzusha. Mwisho wa kunukuu. Watu wa sunna (wanaofuata mafundisho ya Mtume) wanamthibitishia Mwenyezi Mungu kile alichojithibitishia yeye mwenyewe katika majina na sifa, pasina kupotosha wala kukanusha wala kuuliza namna yake wala kupiga mfano, na wanamkanushia Mwenyezi Mungu yale aliyoyakanusha kwake, na wananyamaza kwa yale ambayo hayakukanushwa wala kuthibitishwa, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuna kitu kama mfano wake, na Yeye ni msikivu mwenye kuona".

Nuru ambayo ndiyo sifa yake Aliyetakasika na kutukuka si nuru ambayo amejikinga nayo, nuru aliyojikinga nayo imeumbwa, nuru ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni nuru inayoendana naye Yeye na dhati yake, hakuna kitu kama mfano wake, na alichokiona Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakikuwa kingine zaidi ya pazia linalokuwa kati ya Mwenyezi Mungu na waja wake.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Ubora na fadhila za matendo mema., Toba