Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi

Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapowaamrisha anawaamrisha katika matendo yale wanayoyaweza, wakasema: Sisi hatuna nafasi kama yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, basi anachukia mpaka anaonekana usoni kuwa amechukia, kisha anasema: "Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapowaamrisha watu amali miongoni mwa amali anawaamrisha kwa jambo ambalo ni jepesi kwao na si zito, kwa kuhofia wasijekushindwa kudumu nalo, na yeye pia anafanya mfano walile alilowaamrisha katika wepesi, lakini wao walimuomba kubebeshwa magumu, kwa kudhania kwao kuwa wana haja ya kuzidisha zaidi katika amali kwa sababu yeye amenyanyuliwa daraja zaidi. Wanasema: Hakika sisi hatuko katika hali kama ya kwako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu amekusamehe yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, basi anakasirika mpaka hasira inajulikana usoni kwake, kisha anasema: Hakika mchamungu wenu zaidi na mjuzi wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mimi, basi fanyeni yale ninayowaamrisha.

فوائد الحديث

Amesema bin Hajari: Aliwamrisha yale mepesi kwao ili wadumu nayo kama alivyosema katika hadithi nyingine: "Amali inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni ile inayodumu".

Mtu mwema hapaswi kuacha jitihada katika amali kwa kutegemea wema wake.

Inafaa mtu kusimulia neema alizonazo kulingana na haja ya kufanya hivyo, ikiwa atakuwa na uhakika wa kutojigamba au kujikweza.

Kilicho bora katika ibada ni kuwa kati na kati na kudumu, si kupita mpaka kunakopelekea kuacha.

Amesema bin Hajari: Mja anapofikia kiwango kikubwa katika ibada na matunda yake hilo kwake linakuwa ni msukumo wa kudumu nazo, ili kuzibakisha neema, na kuzizidisha kwa kushukuru.

Sheria ya kukasirika wakati wa kuvunjwa jambo la kisheria, na kumkemea mwerevu anayestahili kufahamu maana ya jambo endapo atashindwa kufahamu, ili kumchochea awe makini.

Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Umma wake, na kwamba dini ni nyepesi, na sheria ni takasifu na yenye upole.

Hamu kubwa ya Maswahaba katika ibada, na kutaka kwao kuzidisha kufanya kheri.

Kusimama katika mipaka ya sheria katika wajibu na ruhusa, na kuamini kuwa kuchukua jepesi lenye kuendana na sheria ni bora kuliko gumu linalokwenda kinyume na sheria.

التصنيفات

Mtume wangu Muhammad - Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-, Hukumu ya Kisheria., Ubora na fadhila za matendo mema.