إعدادات العرض
1- Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, ispokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni.
2- Umma wangu wote utaingia peponi ispokua atakaye kataa, akaulizwa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani atakaye kataa? akajibu: Mwenye kunitii ataingia peponi na mwenye kuniasi atakuwa amekataa
3- Nilitoka katika kundi la Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tukasema: Wewe ni bwana wetu, basi akasema Bwana ni Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka.
4- Nyanyua kichwa chako na sema yasikilizwe, na omba upewe, na taka utetezi utetewe
5- Nimepewa mambo matano, hajapewa yeyote katika manabii kabla yangu: nimenusuriwa (nimeepushwa) na hofu kiasi cha kutembea mwezi mzima, na imefanywa ardhi kwangu kuwa ni msikiti na ni mahala twahara (safi)
6- Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika
7- Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali
8- na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri
9- Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini
10- Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki