Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki

Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki

Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kukihifadhi, Makuraishi wakanikataza, na wakasema: Hivi unaandika kila kitu unachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu huzungumza wakati wa hasira na furaha? Nikaacha kuandika, nikamueleza hilo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaashiria kwa kidole chake katika kinywa chake, akasema: "Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki".

[Sahihi] [Imepokelewa na Abuu Daud]

الشرح

Amesema Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili nikihifadhi kwa kukiandika, mabwana wa kikuraishi wakanikataza, na wakasema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu anazungumza katika furaha na hasira, na huenda akakosea, nikaacha kuandika. Nikamueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- waliyosema, akaashiria kwa kidole chake kinywani kwake akasema: Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake haitoki ndani yake ila haki kwa hali zote, na katika furaha na hasira. Na alisema Mtukufu kumuhusu Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hatamki kwa matamanio * Si vinginevyo, ila huo ni wahyi anaofunuliwa" [An najm: 3-4].

فوائد الحديث

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekingwa katika yale anayoyafikisha kutoka kwa Mola wake Aliyetakasika na kutukuka, katika furaha na hasira.

Pupa ya Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kuihifadhi sunna na kuifikisha.

Kufaa kuapa hata kama hakuna masilahi katika hilo, kama kulitilia mkazo jambo.

Kuiandika elimu ni katika sababu kubwa zinazoihifadhi elimu.

التصنيفات

Umuhimu wa sunnah naNafasi yake., B-Kuzirikodi(kuchapa) Sunnah Za Mtume:, Mtume wangu Muhammad - Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-